Je, watu weusi wanaonewa?

Je, watu weusi wanaonewa?

dungune

Member
Joined
Nov 10, 2021
Posts
70
Reaction score
157
Kumekuwa na malalamiko yanayo tafsiri ubaguzi kwa watu weusi.

Wiki moja iliyopita moja kati ya matukio yalio shika vicha vya habari ni pamoja na tukio linalo onyesha mchezaji wa club ya westham Kurt Zouma akimpiga mateke paka wake.

Umoja wa haki za wanyama umetafsiri kitendo hicho kama ukatili na uvunjifu wa sheria ambapo mchezaji huyo ametakiwa kulipa faini ya ponds.250000 pamoja na adhabu hiyo baadhi ya makampuni yametangaza kusitisha kufanya kazi na mchezaji huyo..

Lakin watu mbalimbali wameonesha hisia tofauti na wengine wakienda mbali na kusema ni kwasababu ya rangi yake ndio iliyochangia kupewa adhabu kali ambayo inaonekana kama ni kubwa kulinganishwa na tukio lenyewe..
Swali langu ni je watu weusi wanaonewa?

Kwanni kumekuwa na malalamiko ya kuonewa hata kama mtu alipatikana na hatia? Ushauri wangu kwa jamii ya watu weusi hasa wanaishi au kwenda ughaibuni tuachane na dhana hii ya ubaguzi bali tuwekeze zaidi kwenye kujijenga.

Mara zote huwa nasema mtu mweusi kweny nchi zinazokaliwa na jamii ya watu weupe ni mgeni haijalishi amezaliwa hapo au alikwenda tu na ukiwa mgeni lazima ufate taratibu za mwenyeji wako.

Akisema kula ni saa kumi jioni na saa kumi usiku itabidi ukubali ukishidwa rudi kwako ukaishi unavyo taka.

HIVYO jamii yote ya Africa tuwekeze zaidi kweny kujenga bara letu ili tuweze saidia na ndugu zetu walio pelekwa huko wakati wa ukoloni.

Screenshot_20220214-154616_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom