JE, WAUJUA ULIMWENGU UKUPAO KILA KITU KATIKA KANUNI ZA ASILI ZA MAUMBILE?
Apiov S. Lwiwa, PhD.
UTANGULIZI
Kama ulikua hutambui ni kwamba tunaishi katika Ulimwengu ambao umefungamana, wenye kuongozwa na Kanuni za kimaumbile. Kanuni hizi zinatawala kila kitu na kila mtu. Ingawa Ulimwengu huu una ‘majaza’ yakutosha yaani Matrix Universe! Ulimwengu ambao unaweza kuaminishwa nyeupe kuwa nyeusi na kinyume chake ikawa sahihi.
Hata hivyo, pamoja na mambo yote hayo, bado unayo nafasi ya kutuliza akili na kung’amua uhalisia wa mambo.’ Ni katika Akili hiyo tulivu yaani attentive mind, ndipo unaweza kufanya Vumbuzi na gunduzi mbalimbali, hata zile kanuni kuu za Kisayansi —katika Quantum Mechanics/Physics. ‘Ugatuaji’ wa maarifa kutoka katika Asili, hutugemea interests au mapendeleo ya mtafuta maarifa.
Majaza’ ninayozungumzia ni kuwa mambo mengi yaliyopo Katika Dunia hii yamekuwa yakubuniwa tu. Kilicho Original ni asili yenyewe yaani ‘Nature’. Ni katika hiyo Asili ndimo kuna Kanuni Asili ambazo ukizijua na kuzifuata, basi utafanikiwa sana hapa Duniani na Ulimwenguni kwa Ujumla. Kwa maana kikanuni hakuna kilichotengana na kingine, kila kitu kipo ndani ya kila kitu. Ingawa kila kitu sio kila kitu kwa “essence” au Uasili wa kitu chenyewe. Twende taratibu. Sisi ni Ulimwengu mdogo, unashangaa? Yes, we are. (Tutaendelea na dhana hii mbele kidogo).
Asili hutupatia kila kitu tutakacho, kwani hakuna kitu chochote tutumiacho, iwe cha kiwandani au Shambani, ambacho hakitokani na Asili. Tunapata malighafi zote za kuunda bidhaa mbalimbali kutoka katika Asili. Sishangai ni jinsi gani sisi na Ulimwengu ni kitu kimoja.
Asili ya Asili ni utulivu. Busara au Maarifa yanapatikana katika utulivu. Je, unataka kushinda jambo lolote? Basi kuwa mtulivu na mkimya. Ukimya una nguvu, kwa sababu ndio asili ya Asili. Ukiwa mtulivu, maarifa yatakufuata kama mtu Tigris uufatavyo mkondo wa Bahari.!
Katika Historia ya maarifa, Mwanafikara Mashuhuri Hermes, aliwahi kuja na Kanuni zake ziitwazo Kanuni za Hermes yaani ’’Hermetic Principles”, ambazo zimeeleza jinsi gani ulimwengu huu una Kanuni za kimaumbile. Zipo nyingi, ila leo nitachambua Kanuni mbili tu:
1. As Above so Below au As Below so Above
2. Principle of Vibration au Kanuni ya Mtetemo
Katika kanuni hii ya kwanza, tunaona kuwa, Sisi ni Ulimwengu mdogo yaani- ’’We are Micro-Universe” and we are all connected kama utando wa buibui.!
Natumia neno Ulimwengu kwa kuwa katika huu uso wa Dunia tuliopo, tunaweza kujihisi tupo peke yetu, katika anga lote, la hasha! Juu yetu, kuna maumbile mengine makubwa ya Asili— Sayari, matufe na Vitufe mamilioni kwa mamilioni. Kwa mfano tunaambiwa kuna zaidi ya Ulimwengu wenye Sayari kama zilizopo katika mfumo-Jua au (Solar System) kwa Mamilioni huko angani. Na hii ikushangaze kufahamu kuwa maumbo hayo ya angani hutuathiri na tunategemeana nayo kila siku na kila mara.
Hii ndio sababu, Wataalamu wa Elimu ya Nyota na Unajimu ( Astrology) ambayo kwa sasa imekua ni (Esoteric Knowledge); iliyopigwa marufuku kufundishwa katika Vyuo Vikuu vingi Duniani, imebatizwa jina la “Astronomy” kama kisaidizi muhimu cha mambo ya Fizikia ya anga; wanaamini kwamba kila mtu anapozaliwa, anakua na ishara yake angani kwa Nyota maalumu ambayo ndio ita-influence maisha ya huyo mtu. Unashangaa? Kwa wale Wakristo na Wasomaji wa Biblia, tafadhali rejeeni tukio la Mama Jusi wa Mtoto Yesu jinsi walivyojua juu ya uwepo wake. Je, unayo maarifa ya kutosha ya kujua jinsi gani Uhusiane na Universe ili kung’amua ukweli huu? Ushawahi kujiuliza ni kwanini watu wanasherehekea “Full Moon” party hasa kule Zanzibar? Ushawahi kujiuliza ni kwanini Maumbo haya—Mwezi, Jua, Nyota nk. Hutumika kama alama za Dini, Taasisi na Mashirika/Makampuni mbalimbali Duniani? Ni lini ulikuja kujua kuwa majina ya Sayari karibia zote ni Majina ya Miungu ya Kigiriki au Kiroma? Ulikua wapi kutambua kuwa logo na majina ya Vumbuzi nyingi za Kisayansi yanapewa majina ya Miungu ya kale? Elimu ya namba je?
Mambo haya na mengine mengi, yanadhihirisha ni jinsi gani tulivyofungamana na kuingiliana na maumbile ya Ulimwengu.
Mpenzi msomaji, sasa tuhamie Kanuni ya pili ya:
Kanuni ya Mtetemo (Principle of Vibration)
Kanuni hii inasema kwamba kila kitu; kinachoonekana na kisichoonekana kinatawaliwa na Kanuni hii. Iwe maada (matter) nishati (energy) kila kitu.
Kipimo cha Kanuni hii ni Hertz (Hz). Unatetema kwa frequence ngapi? Kanuni hii ndio ambayo inahusika na mvutio au ‘attraction’ yaani ukitetema katika ‘negativity’ basi uta ‘attract negativities’ na kinyume chake ni sahihi. Lakini pia, hata kufanya kitu kuonekana au kusikika, kunategemea level yake ya mtetemo. Kuna vitu vinatetema kwa kiwango cha juu sana kupita uwezo wetu wa ku ‘comprehend’ au kupokea, vivyo hivyo, vipo vinavyotetema kwa viwango vya chini mno kiasi kwamba hatuwezi pia kuona au kusikia chochote.
Si ulijifunza au kuwahi kusikia Kanuni ya Kifizikia kuwa everything moves, hakuna kilichokuwa kwenye mwendo? Ndiyo hivyo hivyo huko ku move ni kutetema.
Kutetema huku kunakwenda hadi katika maumbile madogo kabisa ya Atomi (Atom) au hata hadi katika Quants (Quantum Physics) ambapo unakutana na vitu kama mvuke au Waves tu..! Vitu vyote hivi hutetema katika level hizo zisizoonekana kwa macho ya kawaida.
Na hivi nachelea kusema kwamba, hata milima mikubwa, hutetema na kumove….(Unaona haisogeagi sio?) 😃😃 lakini inatetema.
Hapa ukweli ni kwamba, kitu kikiwa kikubwa sana, huwezi kukiona au ku-ki-Comprehend, vile vile kikiwa kidogo sana.

Tutaendelea na Uchambuzi wa Kanuni zingine kwa kadili muda utakavyoturuhusu katika matoleo yajayo ya Makala hii.
Nikutakie makaribisho mema ya mwaka mpya, kama inavyoonekana katika Kalenda ya Mt. Gregory Mkuu, Mwaka Ujao ni 2025.
Happy New Year.!
Apiov S. Lwiwa, PhD.
Daktari wa Shahada ya Falsafa katika Falsafa.