Jukumu la Msingi na Kazi za Benki Kuu
Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
Kazi Zingine za Benki Kuu
> Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania.
Hapa benki kuu huwa ndio inayotoa order ya ku-mint pesa ya Tanzania, pia kuziweka kwenye mzunguko
> Kusimamia mabenki na taasisi za fedha
> Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini
> Kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
> Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
> Benki ya Serikali,
Ni benki ya serikali kwa maana ya kwamba ndio inayohusika na malipo na mauzo ya serikali. Ni benki kuu ndio huuza na kununua amana za serikali, T-Bills and T-Bonds
> Benki ya Mabenki.
Hapa benki kuu ndio hupokea deposits za mabenki ya mengine, pia hutoa mikopo kwa benki hizo