Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Himaya ya Misri ilianza miaka mingi sana. Ilianzishwa mwaka 3000 kabla ya kuzaliwa Yesu. Huo ulikuwa utawala wa mwanzo wa kujenga dola. Utawala wa mwanzo ukaisha mwaka 2700 hivi kabla ya Yesu.
Kuanzia mwaka 2700--2200 kabla ya Yesu kukawa na utawala unaoitwa wa kale(old kingdom). Huu ndiyo wakati mapiramidi Mengi na makubwa ya Misri yalijengwa. Piramidi kubwa la Giza lilijengwa wakati huu na pharaoh Khufu.
Kuanzia mwaka 2180--2055 BC kulitokea kipindi cha machafuko, vita nk.
Kuanzia 2040--1782 BC kukawa na utawala wa nyakati za kati(Middle kingdom). Kumbuka kuwa toka hapo mwanzo hadi sasa watawala wote walikuwa ni waafrika weusi. Lakini mwishoni mwa kipindi hiki watu kutoka mashariki ya kati wakaanza kuingia Misri. Na Misri ilipata pharaoh wake wa kwanza kutoka mashariki ya kati katika wakati huu. Mwishoni mwa Kipindi hiki ndipo waebrania waliingia nchini Misri.
Kuanzia mwaka 1650--1550BC kulitokea kipindi cha vurugu sana na watu kutoka mashariki ya kati(levant) wakavamia Misri na kuweka utawala wao. Walitawala upande wa kaskazini lakini bado upande wa kusini ilitawaliwa na wamisri wazawa. Wavamizi hao wanaitwa Hyskos.
Kuanzia mwaka 1550--1077BC kinaitwa kipindi cha utawala mpya. Hapa watawala kutoka mashariki ya kati walitimuliwa na kilikuwa kipindi cha mapharaoh mchanganyiko, weupe, weusi na machotara. Ni katika kipindi hiki ndipo waebrania walitoka Misri.
Kuanzia mwaka 1000--300BC kilikuwa kipindi cha mambo mengi, wanubi walivamia na kuanzisha utawala unaoitwa black pharaohs. Wakafukuzwa, nchi ikagawanyika hadi mwishowe kuja kuanzishwa kwa utawala wa wagiriki. Mmoja wa watawala hao wa kigiriki alikuwa ni Cleopatra.
So hapa inaonyesha kuwa.
1. Japo Misri ilikuwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa mapiramidi na majengo mengine karibu katika kipindi chake chote. Lakini ujenzi wa mapiramidi na piramidi kubwa kuliko yote lilijengwa miaka 700 kabla ya waebrania kuingia Misri.
2. Mapharaoh wa mwanzo, waliojenga mapiramidi makubwa na kwa miaka kama 1200 walikuwa ni weusi.
3. Ni kweli Misri ilikuwa na mapharaoh weupe lakini walikuja baadaye kama wavamizi.