Halafu ukishajua?? Kimsingi ishu sio umetengeneza ajira ngapi bali ni namna ulivyozitengeneza. Hivi unadhani hao wanaoitwa mafisadi wametengeneza ajira ngapi kutokana na ufisadi wao? Nao tuwapongeze kwa kutengeneza ajira kwa pesa za wizi?
Ninaamini lengo la kuleta mada hii ni zuri kabisa, na kama sijakosea ninaamini ni kuwatia watu motisha wa kufanya kazi zaidi. Hata hivyo huwezi kukataa ukweli kuwa kuna uzembe mkubwa unaendelea serikalini. Hivi vitu viwili ulivyojaribu kuviunganisha havihusiani kwa namna unayotaka tuamini.
Mwisho napenda kusema ni vizuri kuleta motisha wa kazi lakini pia acha tuibane serikali vilivyo.