Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Je wewe ni muhanga wa kufungiwa kutumia Whatsapp Kwenye simu yako na kila ukijiunga Whatsapp lazima upigwe ban ? Unafanyaje kujiondoa?
Wengi wanajiuliza inakuwaje imenitokea hii inakutokea kwa sababu umevunja sheria na taratibu za Whatsapp ndo maana umefungiwa namba yako kutumia Whatsapp.
Kuna aina mbili za kufungiwa kwenye Whatsapp
𝟭. T𝗲𝗺𝗽𝗼𝗿𝗮𝗿𝘆
𝟮. P𝗲𝗿𝗺𝗮𝗻𝗲𝗻𝘁
1️⃣ 𝘁𝗲𝗺𝗽𝗼𝗿𝗮𝗿𝘆
Kawaida unafungiwa kuanzia nusu saa , 1hr ,2hr, 8 mpaka 24hrs. Ila baada siku au masak kadhaa unarudishiwa akaunti yako na kuendelea kutumia kama kawaida.
2️⃣ 𝗽𝗲𝗿𝗺𝗮𝗻𝗲𝗻𝘁
Hii ikikutokea bhana daah inabidi ufanye kazi kidogo maana huwa unafutiwa chati zako , alafu ukijiunga unakua kama unaanza upya vile maana unaondolewa kwenye ma groups yote uliyokuwepo kwenye Whatsapp.
𝗦𝗮𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗚𝗮𝗻𝗶 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗸𝘂𝗳𝘂𝗻𝗴𝗶𝗮
• Kutuma sms nyingi kwa watu kwa wkati mmoja
• Kutuma sms inayojirudia rudia kila mara ndani ya kipind kifupi
• Kutumia app zingine za Whatsapp gb , fm nk
• Kutengeneza ma groups mengi ya Whatsapp ndani ya muda mfupi
• Kutuma link zisizo salama kwa watu
• Kupigwa block na watu wengi inaonekana sio mtu mzuri kwenye jamii.
Jinsi ya kunondokana Permanent Ban
Kwanza tumia 𝗪𝗵𝗮𝘁𝘀𝗮𝗽𝗽 𝗼𝗳𝗳𝗶𝗰𝗶𝗮𝗹 toka soko la play store alafu ukimaliza Sasa inabidi ufanye mambo yafuatayo ili kuwa salama 👇
Kama umepigwa Whatsapp Permanent Ban fanya hivi chukua hii email ya 𝘀𝘂𝗽𝗽𝗼𝗿𝘁@𝘄𝗵𝗮𝘁𝘀𝗮𝗽𝗽.𝗰𝗼𝗺
Kisha fungua email yako usitumie email hii 👇
𝘀𝘂𝗽𝗽𝗼𝗿𝘁@𝘀𝗺𝗯.𝘄𝗵𝗮𝘁𝘀𝗮𝗽𝗽.𝗰𝗼𝗺 haifanyi kazi utakesha.
Fungua email yako kisha andika kuwa unajua umekosa kuwa uliweza kufanya jambo ambalo ukutegemea kama utafungiwa akaunti yako kisha tumia hii email kuwatumia changamoto yako
𝘀𝘂𝗽𝗽𝗼𝗿𝘁@𝘄𝗵𝗮𝘁𝘀𝗮𝗽𝗽.𝗰𝗼𝗺
Baada ya saa 4 mpaka 24hrs pia unaweza kupelekwa ata siku mbili tatu kuweza kufunguliwa akaunti yako hakikisha unaweka na namba ya simu ambayo imefungiwa kutumia Whatsapp.
Jitahidi kutumia official Whatsapp ni salama kwako kuliko Gb Whatsapp?? Vipi wewe ukipigwa banned unafanya kitu Gani tuachie maoni yako?
Credit: Bongo Tech