Je, WWI ilipiganwa katika Ardhi ya Tanganyika?


Unachanganya mambo, umeandika kuhusu MV Liemba ambayo ni meli iliyokuwa inahudumia Ziwa Tanganyika hiyo haina uhusiano na Vita iliwekwa kabla hata ya vita kuanza na haikuwa Meli ya Kivita iliwekwa pamoja na kukamilika kwa reli inayounganisha Pwani na Bara leo tunaita reli ya kati na Kigoma ikiwa mwisho wa reli na pale Kigoma pakajengwa Bandari pia yote yalikuwa maendeleo ya kujenga infrastracture na siyo vita hata Ziwa Tanganyika ambapo Liemba ipo mpaka leo hii ni mbali kidogo na Rufiji delta ambapo vita ilifanyika.

Hivyo liemba haina uhusiano na vita na iko Ziwa Tanganyika!
 
Aah nilichanganya kweli, haikuletwa sababu ya vita lakini ilipigana vita hivo ina uhusiano na vita kwa maana ya kwamba ilishiriki vita lakini haikuletwa sababu ya vita

Vichwa vina mambo mengi mkuu
 
Vita haikupiganwa Rufiji tu. Hata huko ziwa Tanganyika ilipiganwa. Wajerumani waliibadili hiyo Liemba kuwa meli vita na ikawa inatawala ziwa Tanganyika. Waingereza walileta boti mbili, zikapita Congo ya wabelgiji hadi ziwa Tanganyika. Lengo ni kupambana na Liemba. Wajerumani walipoona mambo magumu wakaizamisha. Baadaye waingereza wakaiopoa na hadi sasa inafanya safari ziwa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…