Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,959
- 24,935
Kwanza naomba niombe Radhi kwa wale ambao watachukizwa na Andiko langu pia naomba pia vile vichwa vilivyosomea mambo ya dini vikija vije na majibu yenye fact na sio kutishana,
Je yaliyomo kwenye vitabu vya Dini vyote ni kama Hadithi za Ekaya za Abunuasi ?
Mwanzo kabla Ya wazungu kuja Africa mababu zetu walikuwa wanatumia miungu kama ndio mkombozi wao,hakukuwa na dini lakini kila walichoomba walitimiziwa kwa wakati,
Lakini baada ya kuja tu watu jamii tofauti na waafrika eg wazungu na waraabu walikuja na neno DINI ,
Wazungu wao walikuja na Dini ya kikristo na vivyo hivyo waarabu walikuja na dini ya kiislamu,
Kutokana na mafundisho yao waliweza kuwahadaa mababu zetu mwisho wa siku waliweza kupenyeza Dini zao katika jamii zetu,
Tuzungumzie sasa vitabu vilivyoletwa kwa nia ya kutangaza hizo Dini hapo kuna Biblia kwa upande wa kikristo na Quran kwa Upande Wa islam,
Ukifatilia maandiko yake yamejaa hadithi tena zile Hadithi za kale ambazo kwa upande mwingine unaweza kusema ni hadithi zilizotungwa kwa mpangilio furani,
Lakini kama ni hadithi kweli kwa nini zitungwe na kusambazwa kwa muktadha wa neno Dini,na je watunzi wa hizo hadithi walikuwa na wana lengo gani kutunga na kuleta hadithi hizo?
Vitabu vyote kwa upande wa islam na Christian zina hadithi zinazofanana 95% kasoro majina ya wahusika na Maeneo yake lakini ukivisoma kwa ufasaha utagundua ni kama mtunzi alikuwa mmoja lakini akavitofautisha kwa ustadi mkubwa sana kama ni kweli kwa nini avitofautishe?
Binafsi nina imani katika Mungu lakini sina imani katika Dini kwa sababu moja tu Mungu alikuwepo toka enzi ata kabla ya kuletwa kwa dini.