Je, Yanga kumpoteza Gamondi na Max!?

Gamondi ameboresha sana mbinu za ufundishaji watamtaka TU nawajua wale
 
Kwenye mpira haiko hivyo. Gamondi akifanya vizuri na Yanga champions league hata hao Ahly watataka kuwa naye hakuna linaloshindikana. Kwani kilichowafanya wamchukue kocha Pitso na mchezaji Percy Tau toka Mamelody ni nini?
Point [emoji120][emoji120]
 
Maxi hawezi kuondoka mwakani wala Gamondi. Ila baada ya hiyo miaka miwili inawezekana. Na hilo sio ajabu kutokea kwenye mpira.

Hii Yanga itavurugwa tu labda siku akiondoka Gsm na Eng Hersi Said akichukuliwa na mama namba moja akaitumikie nchi.
Mama ndio tishio kwa sasa [emoji848][emoji848]
 
Walitufunga 5 tukiwa pungufu wwchezaji 2,timu yenyewe ilikua mbovu na tulikua ndani ya mgogoro,wao tumewafunga ikiwa hiki ndio kikosi chao cha dhahabu wanachotamba nacho na kudanganyana wao timu kubwa afrika 😃
Tuwapige nyingi nyingine wafunge midomodomo kabisa Mimi wananiudhi Simba midomodomo mingi wanaongea sana hadi wakandwe tena hata 10 hivi ndio watashona midomo na walie zaidi
 
Walitufunga 5 tukiwa pungufu wwchezaji 2,timu yenyewe ilikua mbovu na tulikua ndani ya mgogoro,wao tumewafunga ikiwa hiki ndio kikosi chao cha dhahabu wanachotamba nacho na kudanganyana wao timu kubwa afrika [emoji2]
Huu ni ukweli hawataki kusema wanaficha sana na mashabiki wao wengi hawajui
 
Derby ya boca junior na river plate sio ya kitoto ni mechi haswa
Derby ya wahuni duniani, mashabiki wauzaji na watumia mihadarati. Ukipoteza mechi kizembe inabidi ulinzi uimarishwe vinginevyo unakula risasi.
 
Derby ya boca junior na river plate sio ya kitoto ni mechi haswa
Ile ni vita na ndio Gamond kachukua technic huko Ahmed akaona jamaa anafanya masihara kumbe yuko serious
 
Aende tu.. Yanga kwa sasa wako kibiashara zaidi.

Aliondoka Fey mkasema
Alivyo ondoka Mayele ...ndio mkasema sana
Alivyoondoka Nabi...Mama Yangu ndio mlichonga sana mpka mijini pale msimbazi ikawa inacheka hazarani.
Asilimia nyingi ya tunaojadili hapa ni wanayanga kwa upande wa madunduka hawana nguvu ya kusema chochote.

Sema kiuhalisia timu yoyote haipendi kupoteza kocha au mchezaji wake mzuri. Hakuna aliyefurahishwa na maamuzi ya Fei, hakuna aliyefurahishwa na kuondoaka kwa asilimi 90 ya benchi la ufundi lililoipa mafanikio timu yetu, hakuna aliyefurahishwa na kuondoa kwa Mayele au kiburi cha Bangala kilichomfanya auzwe Azam. Timu yoyote ili iendeleze ubabe lazima ibakize watu wake bora.

Hivyo kuzungumzia nini kitafuata baada ya mafanikio yetu sio dhambi maana ndio kinachofuata. Hii Yanga ni bora sana kuanzia management, benchi la ufundi, wachezaji pamoja na mashabiki ambao wamekuwa very royal kwa timu muda wote. Ipo siku benchi la ufundi na wachezaji wakitoa huduma nzuri Yanga wapo watakaukuja kutaka huduma yao. Dunia iko hivyo siku ingawa ni ngumu kumeza.

Maxi ana miaka 23 atakapomaliza miaka yake ya mkataba atakuwa na miaka 25 atakuwa mwanaume amekomaa mno. Kama atakuwa na kiwango hiki alicho nacho sasa ama kuongezeka basi wenye nguvu watamtwaa na hatutakuwa na uwezo wa kumzuia.

Jambo la msingi kwa sasa tuna uongozi thabiti na udhamini bora. Tuko mikono salama kwa sasa
 
Wenzenu wameshafukuza kocha huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…