Je yanipasa kulipa kisasi???

Je yanipasa kulipa kisasi???

sixlove

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
563
Reaction score
393
Ndugu zangu wa jf, hapo kitambo nilikuwa na girlfriend, mwanzoni mahusiano yetu yalikuwa bomba kabisa na nilitokea kumpenda hasa pale alipofanikiwa kunifanya nisivute sigara,,na kweli baada ya muda mfupi niliacha kabisa kuvuta sigara, cha kushangaza baada ya muda mfupi tabia yake ilianza kubadilika ghafla tena baada ya kumtambulisha kwa rafiki yagu ambaye tumeshibana sana, kutokana na mambo mengi ambayo tumekuwa tukifanya pamoja. ugomvi wa mara kwa mara uliendelea kutawala uhusiano wetu huku yeye na huyo rafiki yangu wakionekana kupatana sana kiasi cha kutembeleana hata mi nisipokuwepo. Mahusiano yalinishinda nikaamua kuvunja uhusiano naye.

Cha kushangaza hivi majuzi nimepata habari iliyonishtua sana, kwamba rafiki yangu huyo alikuwa ana date na mpenzi wangu, ilihali ana girlfriend wake ambaye anampenda sana jamaa na mara nyingi wakigombana huwa anakuja kuomba ushauri kwangu na mambo yanaenda fresh. ndugu wana jf kumbe kwa wakati wote huo nilikuwa napigana vita na adui nisiye mfahamu, nilipokuwa nahitaji suluhisho kwa mpenzi wangu kumbe nilikuwa najichoresha kwao, huku kwa nyuma wakinicheka. JE YANIPASA KULIPA KISASI KWA MIMI KUMCHUKUA DEMU WA JAMAA LIKE WHAT HE DID? Naombeni ushuri wa kina kabla sijatoa uamuzi
 
6Love pole saana.... Mie naona la msingi hapo ni kwamba your friend in some way alionesha the type of woman Mpenzi wako alikua.... Mie naamini kua sometimes muitikio wako kwa mwanaume ndo hufanya akutongoze ama lah! Kama kweli mpenzi wako angekua anakupenda asingemkubali jamaa ambae ni rafiki yako. Na kama ujuavo ni wanaume wachache ambao hupotezea kulala na mwanamke ambae kakubali kujirahisi kwake no matter ni gal friend wa rafiki/jirani/kaka ama mdogo.... Woote wawili (your ex na rafiki wako ) wana makosa for sidhani kama binti alikua ni mtoto mdogo na kwamba alikua hana maamuzi.... After all kama aliweza kukuachisha sigara... Alikua na uwezo wa kumkataaa rafiki yako kama kweli alikua anakupenda. Mbaya zaidi kukuchoresha kwa kukaa vikao.... That was so unfair and bad of them....
 
hapana bro usilipize kisasi,nachokushauri mimi wapotezee wote huyo x-girlfrnd wako na huyo rafiki yako,wewe endelea na mishe mishe zako za maisha.cuz malipo n hapa hapa dunia na wala uhitaji kulipiza kisasi bali mungu ndyo atakulipia.kuwa free,peace na relax kwa kukalibisha mwaka mpya na mambo mapya bro.dnt revenge bro na usimuchukue huyo demu wa rafiki yako.
 
What is the purpose of kisasi?Ili iweje?Halafu hicho kisasi ndo kitafuta hiyo kadhia?Achana nao we endelea na maisha,simaanishi umchukie rafiki yako!
 
Ukifanya kitendo kama hicho, utaonyesha maamuzi yako ni ya kitoto. Wewe unatakiwa uonyeshe tofauti kati ya hao wawilli, kwamba wamefanya upumbavu, lakini wewe huko tayari kufanya kitendo kama hicho. Achana nao. Muombe Mungu atakupa binti ambaye mtajenga familia kwa pamoja.

Ubarikiwe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hakuna haja ya kulipiza kisasa
huyo girl hakuwa anakupenda kwa dhati
ukilipiza kisasi wapata faida gani
alichotenda ndicho kinachokuumiza hata ukilipa kisasi
bado ndani ya moyo wako utakuwa unaumia
subiri utapata anayekupenda na kukuthamni
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Furahi umepata nafasi ya kumjua huyo dada vizuri mapma kabla hamjafika mbali zaidi. Shukuru alafu mpotezee dada au hata wote wawili.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
a true winner z nt who fight and win z th one who can be beaten n still can gt on his/her feet an keep going on no matter how many hits he/she get and how hard he get hitted...you r a true winner mkuu ,dnt loz ur reputation and dignity ww endelea na maisha yako achana na hao ila its better uongee nao ili wajue kuwa umeshajua wat thy r doing.
 
Sikushauri kabisa kulipiza kisasi, wewe wapotezee tu na siku moja Mungu atakulipia mbele ya macho yao. Pole sana bro.
 
aseeee.....sasa fanya hivi...., I mean,
chukua time....
 
toba yalaaa....mkamaye umchakachue huyo dem wake ikiwezekana piga mimba kabisa
 
nashukuru sana ndugu zangu wana JF, kwa nasaha mlizotoa na mtakazoendelea kutoa. Siko mbali na ushauri mlionipa na sasa natarajia kufanya kama mmoja kati yenu alivyonishauri.

Nitawaita wote( x-girlfriend wangu, rafiki yangu, marafiki zangu wote nilonao hapa chuoni, demu wa jamaa) na kuwaeleza yaliyotokea kisha, kisha KUWASAMEHE kama jinsi mungu na binadamu wengine wanavyonisamehe, then. I WILL BE A FREESOUL.

NAWAPENDA SANA NDUGU ZANGU,,,,,HAKIKA MUNGU AMENIKUTANISHA NA JAMII MPYA
 
nashukuru sana ndugu zangu wana JF, kwa nasaha mlizotoa na mtakazoendelea kutoa. Siko mbali na ushauri mlionipa na sasa natarajia kufanya kama mmoja kati yenu alivyonishauri.

Nitawaita wote( x-girlfriend wangu, rafiki yangu, marafiki zangu wote nilonao hapa chuoni, demu wa jamaa) na kuwaeleza yaliyotokea kisha, kisha KUWASAMEHE kama jinsi mungu na binadamu wengine wanavyonisamehe, then. I WILL BE A FREESOUL.

NAWAPENDA SANA NDUGU ZANGU,,,,,HAKIKA MUNGU AMENIKUTANISHA NA JAMII MPYA
pamoja mkuu ,ila siyo lazima kuwaita marafiki zako wote ....nyie wanne(u ,ur x,ur frend n ur frends gal) au watatu(u ,ur x n ur frend) mnatosha kuelezana ukweli usifanye big issue sana hapo kaka.
 
we songa mbele na maisha ukuzaliwa nao wote wawili..mwanamke asikufanye upagawe na kugombana na msela we kata mawasiliano na wote wawilli huyo mwanamke ni cheeeep kama fungu la dagaa shukuru mungu umemtambua mapema angekuletea kisonono ndani.......mi nikishahisi mwanamke anatabia ya uwongo wa mapenzi faster natupa baharini kwenye MAMBA .....
 
cha kwanza jipende wewe.
Kulipa kisasi ni kuufunua mwili wako kwa mtu mwingine ambaye hutegemei kuwa na future naye.
Tuliza akili, tafuta mwingine anayekufaa.
 
...Songa mbele na maisha Mkuu. Utapoteza wakati wako bure na pesa zako nyingi kwa kitu ambacho hakina maana yoyote (kulipiza kisasi). Huyo binti wa rafikiyo si ajabu hata mapenzi naye huna ila tu unataka kuwa naye ili kumkomoa rafiki yako. Achana naye huyo si rafiki wa kweli maana rafiki wa kweli hata siku moja hawezi kufanya hayo aliyoyafanya. Kila la heri katika kufanya maamuzi yenye busara.
 
Umeshasikia kitu kinaitwa 'Gusa Unate'?

Unawasha kama switch ya taa naye anawaka hapo hapo, ukichoka unazima switch anazimika hapo hapo

Labda anamjua ni gusa unate

Je, unaweza tu kumchukua huyo demu bila yeye naye kukutaka wewe?
 
Pole sana sixlove, wapotezee na uendelee na maisha yako, haina haja ya kulipiza kisasi! Jichanganye sana na marafiki ili uweze kusahau yalotokea. Ipo siku utampata wako Mungu atakusaidia na utaishi maisha mazuri sana!
Pia mshukuru Mungu kwa kukuonyesha mapema ya kuwa huyo x wako hakufai, hivyo yakubidi umuombe akupe mke/mwanamke wako!
 
Back
Top Bottom