sixlove
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 563
- 393
Ndugu zangu wa jf, hapo kitambo nilikuwa na girlfriend, mwanzoni mahusiano yetu yalikuwa bomba kabisa na nilitokea kumpenda hasa pale alipofanikiwa kunifanya nisivute sigara,,na kweli baada ya muda mfupi niliacha kabisa kuvuta sigara, cha kushangaza baada ya muda mfupi tabia yake ilianza kubadilika ghafla tena baada ya kumtambulisha kwa rafiki yagu ambaye tumeshibana sana, kutokana na mambo mengi ambayo tumekuwa tukifanya pamoja. ugomvi wa mara kwa mara uliendelea kutawala uhusiano wetu huku yeye na huyo rafiki yangu wakionekana kupatana sana kiasi cha kutembeleana hata mi nisipokuwepo. Mahusiano yalinishinda nikaamua kuvunja uhusiano naye.
Cha kushangaza hivi majuzi nimepata habari iliyonishtua sana, kwamba rafiki yangu huyo alikuwa ana date na mpenzi wangu, ilihali ana girlfriend wake ambaye anampenda sana jamaa na mara nyingi wakigombana huwa anakuja kuomba ushauri kwangu na mambo yanaenda fresh. ndugu wana jf kumbe kwa wakati wote huo nilikuwa napigana vita na adui nisiye mfahamu, nilipokuwa nahitaji suluhisho kwa mpenzi wangu kumbe nilikuwa najichoresha kwao, huku kwa nyuma wakinicheka. JE YANIPASA KULIPA KISASI KWA MIMI KUMCHUKUA DEMU WA JAMAA LIKE WHAT HE DID? Naombeni ushuri wa kina kabla sijatoa uamuzi