Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Baada ya kuanguka ghorofa huko Kariakoo chanzo kinadai mmiliki alitaka kuchimba chini ajenge underground floor kwa ajili ya kuongeza fremu za biashara.
Naamini huyu siyo mmiliki wa kwanza kufanya hivi, amefuata nyayo za wamiliki wengi waliotangulia. Naamini pia kwamba majengo yaliyochimbwa chini yanafahamika na wafanyabishara pamoja na mamlaka za serikali
Nipende kufahamu, je serikali ipo tayari kutoa taarifa ya majengo yaliyoathiriwa na tamaa za fedha kama jengo hilo? Je, hayo majengo haliruhusiwa kujengwa?
Jambo la mwisho ni ubora wa majengo, tumeona kabisa zege na NONDO kwenye jengo lililoanguka havina ushirikiano. NONDO chache, cement fupi na kokoto cha chombeza. Je, walioruhusu haya walilipwa nini? Tumeona pia bomoa bomoa ikiendelea na majengo yakichukua chini ya miezi sita kujengwa zaidi ya ghorofa kumi? Je, haya majengo mapya ya NHC na wawekezaji binafsi yanazingatia ubora au yanazingatia kukamilika? Ni nadra sana ghorofa kumi kujengwa chini ya mwaka ila kariakoo ujenzi unachukua miezi mitatu hadi minne kukamilika. Viwango vinazingatiwa?