Je, yawezekana kuwa na taasisi binafsi kupeleleza na kuandaa mashtaka ya jinai?

Je, yawezekana kuwa na taasisi binafsi kupeleleza na kuandaa mashtaka ya jinai?

Sambwisi

Senior Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
175
Reaction score
69
Wakuu, napenda kujua kama inawezekana kwa hapa Tanzania kuanzisha taasisi/kampuni binafsi ya kufanya upelelezi wa makosa ya jinai na hatimae kuandaa mashtaka na kusimamia kesi hizo mahakamani?

Nakuja na swala hilo kwa kuona kuna kesi za jinai (sina takwimu) hata pale ushahidi unapokuwa dhahiri watuhumiwa wanaachiwa huru na mahakama.

Nashawashika kusema kwamba vyombo vyenye mamlaka hayo (Polisi na Waendesha mashtaka) aidha kwa makusudi; kutokuwa na weledi wa fani; kutumiwa na viongozi au kutokana na kukithiri kwa rushwa haviwajibiki ipasavyo. Aidha utakuta jambo halipelelezwi kabisa au upelelezi utakuwa wa kubabaisha na hata pale upelelezi unapofanyika uandaaji wa mashtaka na uendeshaji wa kesi utafanywa kwa kuacha shaka (loopholes) ambazo hatimae mahakama hazitamtia hatiani mtuhumiwa kwa kigezo cha aidha mashtaka kukosewa kwa kutoendana na matwaka ya kisheria kumtia mtu hatiani, au kuwa na ushahidi wenye kutia shaka kwa vile ushahidi inatakiwa usiwe na shaka (evidence beyond reasonable doubt), na mengi mengineyo.

Kama haiwezekani kuwa na taasisi kama hiyo, WaTz tuna maoni gani?

Nawasilisha kwa mjadala zaidi.
 
Maoni yangu ni kuwa, ur idea ni nzuri sana, kama ipo kwaajili ya kuseek 4 someone's justice, itasaidia sana though kwenye upande wa rushwa bado tatizo hilo halitaisha sanasana hongo itakua juu zaidi kuziba midomo ya waheshimiwa. Evidence za kutosha zinapatikana kwenye makosa ya jinai ila tatizo ni sheria kupindishwa huku haki ikionekana wazi ikipindishwa. So iyo taasisi ingedeal na evidence za watakao kula rushwa kwenye kesi pia ili wasipindishe sheria.
 
Back
Top Bottom