Je, Zanzibar inajiandaa kujitwalia uhuru kamili?


Ili iweje?Tukivunja Muungano kuna hasara gani?
 
Ni kweli kabisa, movement ya watu imesaidia kuimarisha muungano, lakini kuna hatari ya vyama viwili tofauti kushika dola Zanzibar na kwenye serikali ya Muungano, jaribu kupata picha mwaka 84 kama Jumbe asingekua mwanachama wa CCM.
 
Muungano ni jinamizi linaloitafuna tanganyika na zanzibar, muungano huu wa shinikizo la wakoloni wa kutekeleza mpango wa udhibiti wa nchi za afrika. Mpaka leo hii hakuna anaejua umuhimu wa muungano na sababu za muungano,sababu zinazotolewa na viongozi ambao wote wanakaririshwa sababu hizo juu ya umuhimu wa muungano ni ulinzi na usalama,sababu ambazo ni za uongo wala hazina mashiko yeyote,umbali wa Kenya na tanganyika ni kama mita moja tu na hakuna tishio la aina yeyote wala hakukuhitajika muungano wa hofu kama ulivyo wa Zanzibar na tanganyika
-Mambo yalitakiwa kudhibitiwa barani afrika ni historia
Nchi ambazo zilikuwa na utawala wenye historia ndefu zote zimepinduliwa na historia zao kuuliwa kabisa Kama ethiopia, Zanzibar na nchi nyengine za afrika

wakoloni walitaka historia ya nchi zote za afrika ianze kwenye kupata uhuru na sherehe za uhuru ziwe jiwe la msingi kwa nchi za afrika,kwa hio ikitokea kama kuna nchi ambao ina historia,utawala na serikali inayopita tarehe za uhuru lazima waiangamize,na Zanzibar ni moja ya hizo nchi ambazo historia yake ya utawala ni mrefu ulianzia na waraabu mpaka masultani wakawa Wazanzibari ambao ni machotara walochanganya kama wazanzibari wa sasa
Ethiopia pia ilipitiwa na kimbunga hiki cha wakoloni wanaodhibiti historia za afrika,utawala wa Ethiopia ulikuwa na zaidi ya miaka 3000 ya ufalme, wakoloni walihakikisha unakufa na historia yake pia,na kuanzisha utawala wa dunia mpya

kwahio muungano wetu hapa ni jinamizi ambalo mpaka viongozi wetu wanachezeshwa ngoma wasioujua mdundo wake,wanageuzwa kuwa maagent wa kuliteketeza bara la afrika,

kwa maana kama watoto wetu hawana kiio cha historia watakuwa hawana morality ya kujielewa na kufanya chochote cha maana
 
hapa umewasingizia wakoloni hawakuhusiki,muungano ulikuwa ni kwa faida ya mwalimu na karume ambao waliangalia suala la ulinzi kw awakati ule ili kudhibiti tishio la sultani wa oman kuweza kurudi kuitawala zanzibar,ambavyo hizi hoja ni mfu kwa karne hii ya kisasa.
znz iachwe iwe huru ijiamulie mambo yake yenyewe tuungane kwenye mengine
 

Rais wa pili wa Tanzania mzee mwinyi alizaliwa kisarawe Pwani.. akaenda Zanzibar na baadae akawa rais wa Tanzania kama mzanzibari.. mwanawe alikuwa mbunge wa mkuranga bara baadae akaenda kuwa mbunge Zanzibar na anaelekea kuwa rais ajae wa Zanzibar.. achana na kina balozi sepetu, wale kina brigedia mwakanjuki kutoka bara wanaitumikia serikali ya mapinduzi.. mwanamapinduzi mzee natepe kutoka mtwara nae kaacha wanawe wanaitumikia SMZ na serikali ya muungano.. hawa wapemba huku tabora washaweka makazi na wamezaa na wanyamwezi achana na hao wapemba wa dsm na wengine waliozagaa kila kona..

Sisi ni ndugu na tumeshachanganya damu sana..kutengana kutawanufaisha tu kwa muda wanasiasa na kuleta sintofahamu kubwa kwa raia wa pande zote mbili..

Tuache mihemko.. tuimarishe muungano .. kero za muungano tukiamua tunaweza kuzitatua!
 
Hapo kwenye muungano kukosa sababu za msingi (at least tunazozijua) naungana na wewe kabisa. Nimepekua sana, sababu kubwa ninayokutana nayo ni 'undugu wetu'.
 
Muungano unaificha Zanzibar kwenye sura ya kimataifa. Ukienda sehemu nyingi duniani jina Zanzibar ni maarufu kuliko Tanzania.
Watalii wanapoenda mahali wanafuata vivutio vya utalii sio majina ya nchi. Pia Zanzibar kama sikosei ina bodi yake ya utalii na pia utalii sio jambo la muungano.
 
Hizi mada hua kuna watu hawazitaki.

Fuatilia kwa undani kwa waasisi wa ASP kule Zanzibar ujuwe yaliyo moyoni mwao.

Tafakari haya.

1. Nini sababu za kifo cha hayati Karume mwaka 1972 mwaka wa 9 kuelekkea muda wa Mwisho uliokusudiwa Muungano uvunjike baada ya miaka 10? fuatilia upate simulizi za kusisimua. Siri ya kifo cha Karume anaijua Mwenyezi Mungu lakini........... Lakini siasa za Muungano zinatajwa.

2. Fitina ya Zanzibar na ubaguzi unaoendelea imesukwa vyema kwa malengo yaliyojificha ya kuimeza Zanzibar. CCM imebeba bango hilo kutoka serikali mbili kuelekea moja.

3. Wazanzibari asili na wana Mapinduzi asili wanacheza karata ya URAIS ya kutaka kupewa MTU wao ili walau wajifariji lakini imekuwa pata potea maana sasa CCM ina utamaduni wa kumpitisha mtu wao kutoka Dodoma. ( CCM asili wanaugulia machungu ya kujitakia) walisahau ajenda ya bara ni kuimeza Zanzibar sasa wamenasa.

4. Ndio huwa tunawashangaa wasiojua Historia ya Zanzibar kumsifu Marehemu Mzee Jumbe. Huyu ndie aliyefanikisha Kuivunja ASP na Kuiunganisha na TANU kuwa CCM. Lakini fitina ilianza miaka ya nyuma ya kuunganishwa Shirazi Association na African Association kupatikana ASP. Mawindo ya Tanganyika kuuwa uzalendo wa Zanzibar yalianzia mbali. Historia ni ndefu lakini Mzee Jumbe alikosana na Mwalimu Nyerere ndio akafukuzwa lakini alikuwa mwana mikakati wa kuidhoofisha Zanzibar.

5. Kuunganishwa kwa ASP na TANU na kupatikana CCM, fuatilia siku hiyo Wazanzibari wazalendo waliokuwemo kwenye ASP namna walivyolia kuuliwa kilichoitwa " AFRO MAMA" ukipata simulizi machozi yatakutoka.

Kwa ufupi Zanzibar tokea wakati wa Mzee Karume hawajawahi kufurahia Muungano huu na wala usibabaishwe na utofauti wa vyama.

Kuna jambo moja hulijui. CCM sasa kwa upande wa Zanzibar iko kwenye mkakati wa kuongozwa na watu waliopandikizwa kutoka Bara na wala sio hao akina Pandu na Jecha tena. Mkakati ni kuondowa vikwazo zaidi ili njia ya kuihodhi SMZ na kisha kuipoteza Zanzibar iendelee.
 
Mkuu umenikosha kwa bandiko lako lililoenda Shule, hii ndo ilikuwa JF ya zamani,

Wenye maono tulitaka Katiba mpya ili kuridhiana ili tuwe na mfumo thabiti wa Muungano. Wakatokea wabinafsi wachache wasioona mbali wakavirunga mchakato wa Katiba mpya.

Ukweli Ni kuwa kwa Sasa hatuna Katiba ya kuulinda Muungano ndani ya mfumo huu wa vyama vingi, kilichopo Ni Bora liende tu.
Mkakati ni Kwa kuibara kura kufuta matokeo, na ubabe wa kutangaza mshindi mtu wao

Ipo siku yaja haiko mbali, watafeli na Muungano itakuwa Basi tena itabaki majuto Ni mjukuu
 
Chama chakavu kikikatwa mtama kama mbasha itakuwa ni furaha sana kwa wale masheikh wanaosota kwa kupinga dhuluma
 
Ikitokea vyama viwili tofauti vikashinda Bara na Visiwani, je Tanzania itabadili jina?
 

Katika wale 'Geniuses' wangu hapa JamiiForums nawe upo kama labda ulikuwa hujui na nakukubali mno ila kwa sababu za Kiusalama acha uwepo.
 
Naam shukrani mkuu kwa nondo hizi.
 
Umesoma historia potofu ktk hili suala la muungano, ukweli ni kwamba Karume ndo alipenda kuwe na serikali/nchi moja ila Nyerere ndo akakomalia serikali mbili tukiri tu hapa nyerere alipotoka alishindwa kuona ya mbele!
Yaa! Ni kweli, nyerere alipoteza fursa adhimu, aliogopa kuonekana mkoloni mpya kwa zanzibar, kwani wakati ule kulikuwa na vuguvugu la ukombozi afrika, na yeye alikuwa msitari wa mbele,

angeulizwa wewe mbona unamwondoa sultan alafu unakaa wewe

Nadhani alifungwa na dhamiri
 
Naam, ni hatari ambayo kila mtu anaiona lakini wanasita kuitaftia ufumbuzi wa kudumu. wakisha iba uchaguzi wanasahau kabisa, baada ya miaka mitano ndio matumbo yanapata joto tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…