Kweli tupu, ila Nchi hii inatupeleka wapi?
nami nasikia sikia kuwa ze comedi wamenunuliwa na mafisadi je wataweza kuwakilisha na kufikisha ujumbe wa walengwa kama wameshanunuliwa??au itakuwa kwa manufaa ya mafisadi?yetu macho
ndio, wamenunuliwa na mafisadi. si uliona jana walipoonyesha wanacheza kwenye jengo la Quality group, jengo la Manji?
Hata hicho kifo cha Wangwe ilikuwa ni sehemu ya Kampeni za CCM Tarime. Reflection ya ujumbe ilikuwa inalenga kusisitiza kuwa aliuawa.
Wakurya sio wafunga misuli na kanzu, mwanaume suriali, kaptula au utupu kama masai.
Hawa vijana hawana jipya tena kwani mengi ya matukio ya kuigiza na kukosoa yapo CCM na serikalini.
Njaa mbaya, pole Origino Komedi kama sio origino komoni.
Mbona tunawaangalia the comedy tu, hawa ni vijana wanaojaribu kutafuta maisha, lizee lizima kaa Mengi kuwawekea kiwingu ni kwa ajili gani, mbona hatumwambii Mengi kuwa awaache hawa vijana na jina hili kwa mapesa aliyonayo atakua amepoteza nini?. Jamani jamani tukiwaacha kweli watanunuliwa
Jamani...
Ze Comedi is still independent under contract with TBC1, Show zao ni Alhamisi,marudio ni J2, just only the slight change of name.
Wangekuwa hawako free sidhani kama wangekuwa na confident ya kuigiza kuhusu kifo cha Wangwe.
Let them do the best they can offer....
Mimi nilishasema huko kwenye thread nyingine tulipokuwa tunachangia suala la hawa mafisadi wadogo.
Najua wapenzi wengi wa ze komedi na hasa fisadi's supporters wanaweza kusema wanavyosema na kuwapamba wanavyopenda.
Hawa vijana wameshanunuliwa na mafisadi na hawawezi kamwe ku perform kama zamani.
Kiwango lazima kishuke tu. Maana hawana uhuru waliokuwa nao ch 5.
Ndiyo sababu wanaweza ku act kifo cha Mengi lakini hawezi kuonyesha kuwa wahusika ni sisiemu wenyewe. Ila wana act mambo ya wakina mtikila tu wakipigwa mawe.
Sasa subiri uone kama wata act sisiemu kushindwa.
Hawa kwisha. Na si siku nyingi tutaacha hata kuangalia upuuzi wao. Labda watabaki wakiangalia mafisadiz na familia zao.
Kwa swala la freedom hata mimi na doubt maana ile TBC1 si ya wenyewe? But can that conclude kwamba wamenunuliwa?
..With binocular au?? Hawajanunuliwa wala nini.. Nyie mnataka wanachoigiza kiwe vipi?It doesn't conclude lakini unaweza kusoma barua ndani ya bahasha
Mkuu kidzogolae;
Orijino Komedy kuigiza mbele ya Quality Group building still sio evidence ilosimamia kucha.
Kwahiyo hao jamaa wakiigiza mbele ya ofisi za Vodacom au kudhaminiwa na Vodacom utasema imenunuliwa na Mheshimiwa R.A?
Plz kama una maanisha unachotetea then leta hoja with evidence...una haki ya kutoa maoni/fikra zako.
Hii orijino komedi, ni feki komedi kwa kusema kweli.
Hivi kuna mmoja wenu aliyeshtuka na jinsi vijitangazo vyao vilivyo kati kati ya onyesho?
Onyesho la kwanza TBC1 walitangaza biashara ya umalaya. Lililofuata sikuliangalia. Hili la jana wametangaza biashara ya utoaji mimba.
Whither Tanzania? Au ni mimi peke yangu niliyeona? Na sijasoma popote katika vyombo vya habari Tz vilivyolalamikia hilo. Pengine ndivyo tulivyo?