Je, ZFF haiitambui kalenda ya FIFA?

Je, ZFF haiitambui kalenda ya FIFA?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
ZFF ni Zanzibar Football Federation kwa Kiswahili ni Shirikisho la Soka la Zanzibar sawa na TFF.

Kimenishangaza ligi ya Zanzibar inaendelea wakati huu ambapo mechi za timu za mataifa zikiendelea.

Timu za Simba na Yanga zimecheza mechi za kirafiki kwa angalizo la kutooneshwa ama kutangazwa kwa sababu hairuhusiwi.

Sasa ZFF ipo vipi?
 
Zanzibar anaonewa
Inatakiwa awe mwanachama kamili wa CAF ashiriki mashindano
Ona vijana wa Zanzibar Jana wametubeba Tanganyika
Bacca
Mudathir
Feisal
 
Wazanzibar na watanganyika wameungana jana timu imecheza na matokeo yamepatikana. Sasa walipoonewa ni wapi mkuuu?
Sasa hapo unataka uhakika Gani?
Tanganyika wameshiriki
Wazanzibar wapo visiwani wanavua kasa
Vijana wao ndo walikuwa mastaa kwenye mchezo
 
ZFF ni Zanzibar Football Federation kwa Kiswahili ni Shirikisho la Soka la Zanzibar sawa na TFF.

Kimenishangaza ligi ya Zanzibar inaendelea wakati huu ambapo mechi za timu za mataifa zikiendelea.

Timu za Simba na Yanga zimecheza mechi za kirafiki kwa angalizo la kutooneshwa ama kutangazwa kwa sababu hairuhusiwi.

Sasa ZFF ipo vipi?
ZFF siyo mwanachama wa FIFA na wala haitambuliki!
 
Mbona na mechi za ligi kuu nbc premier zimechezwa leo kitayoce vs kagera, singida vs kengold ,sijakuelewa mtoa mada unamaanisha nini ? Ligi isimame kwa sababu gani hasa manake mechi za kimataifa mzunguko huu mechi zimeshaisha usiku wa kuamkia leo
 
Na anayewabania ni TFF, ili waendelee kunufaika na pesa za migao ya uanachama peke yao.
Kwa kweli unasikitisha. Hii ni TFF inataka kuimeza ZFF na kuifanya kama chama cha mkoa cha futiboli.
 
Back
Top Bottom