Jean Paul Sartre

Jean Paul Sartre

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Jean-Paul Charles Aymard Sartre Mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchini Ufaransa aliwahi kuandika kumuhusu Ernesto "Che" Guevara, kwamba; “ not only an intellectual but also the most complete human being of our age.”

Ikiwa ni takribani miaka saba baada ya kifo cha Che.

Maneno haya ya muumini kindakindaki wa falsafa ya "Existentialism" bwana Jean-Paul Charles Aymard Sartre yanaungwa mkono na Andrew Sinclair mwandishi wa kitabu cha Guevara; kwamba ni kweli Che alikuwa 'Complete human being' katika hizo zama.

Katika umri wa miaka 39 tu Ernesto "Che" Guevara pekee yake alikuwa na 'career' nyingi pengine kuliko kundi lote la watu katika maisha yao yote.

[emoji1542] A doctor

[emoji1542] A diarist

[emoji1542] Political and military theorist

[emoji1542] A guerilla fighter

[emoji1542] An economist

[emoji1542]A tactician

[emoji1542] A banker

[emoji1542] A planner

[emoji1542] An industrialist

[emoji1542] An ambassador

[emoji1542] A propagandist

[emoji1542] And as the doer of all his other duties.

Sasa ni hivi, Tunafahamu Che alikaa darasani kusomea udaktari wa Binadamu;
Swali kujiuliza, ni lini tena Che alikaa darasani kusomea hizo 'career' zingine zote alizopata kuwa nazo?

Pichani ni Simone de Beauvoir, Jean-Paul Sartre akiwashiwa cha Arusha na Che Guevara walipokutana huko Cuba mwaka 1960.[emoji23]

Mshkaji wako,
Deusy Mwakalinga Jr.

COMMENTS ZA MOHAMED SAID

Deusy wewe mtoto hata sijui unatafuta nini kwangu.

Toka asubuhi mimi nilitambua mapema alfajir kuwa wewe ni mtu matata sana.

Jean Paul Sartre.

Che...

Mimi nakua mjini Dar es Salaam huyu Che na Malcolm X ndiyo walikuwa mashujaa wangu.

Umenikumbusha kwa kumtaja Jean Paul Sartre sheikh na mwalimu wangu Sayyid Omar Abdallah maarufu kwa jina la Mwinyi Baraka.

Katika miaka ya 1980 Muslim Student Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) walifanya seminar Nkrumah Hall na katika wazungumzaji alikuwa Mwinyi Baraka.

Ilikuwa si kawaida wasomi wa Kiislam kuzungunza Nkrumah Hall basi ukumbi ukajaa kuja kushangaa hawa nao wana nini?

Mwinyi Baraka akasimama kuzungumza hadi akamaliza.

Mwinyi Baraka ukimtazama kichwani ana kilemba, kizubao, kanzu na kashda begani.

Haikupitikii kuwa ni msomi wa University of Oxford.

Picha iliyowajia wengi pale ukumbini wasiomfahamu ni sheikh katoka Zanzibar.

Katika kipindi cha maswali na majibu akasimama kijana mmoja na ile ''body language,'' yake ikawa imejieleza yote.

Kwa kiburi na jeuri kijana akamwambia Sayyid Omar Abdallah kuwa dunia ya sasa ni dunia ya ''materialism,'' kijana akatamba sana pale.

Mwinyi Baraka kainamisha kichwa anamsikiliza kwa upole kabisa kijana akamfundisha sheikh, ''Theories of Development,'' kama zinzvyoelezwa na Marxists.

Kijana akamaliza.

Ukumbi ukalipuka, umechangamka, makofi yamepigwa kwa shangwe kama vile kusema, ''Hawa nini wanataka kutuletea mambo yao hapa yasiyokuwa na kichwa wala miguu."

Mwinyi Baraka akasimama kujibu.

Akatoa nukuu ghibu, yaani ''off head,'' ya ukurusa mzima wa Jean Paul Sartre kutoka sura ya kitabu chake kimoja anaisoma ile nukuu kwa Kifaransa.

Ukumbi umeanza kushtuka watu katika hadhira wanatazamana.

Kisha akamwambia yule kijana hayo uliyofundishwa hapa si mambo mapya Jean Paul Sartre alishayasema hayo miaka mingi huko nyuma.

Sheikh akasherehesha kwa kiasi chake.

Akahitimisha kwa kumwambia kijana kuwa mengine awaulize walimu wake ambao wako pale ukumbini watamfundisha.

Mwinyi Baraka akakaa kitako.

Nkrumah Hall ilikuwa kimya.

Ukiangusha sindano utasikia mlio wake.

Kijana aliyeuliza swali kwa kukosa adabu akawa mdogo kama ''piriton.''

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijaelewa ulichoandika unataka kueleza nini.
Laki...
Usikiumize kichwa chako hata mie husoma vitu nikatoka patupu.

Hauko peke yako.
Tatizo hilo wanalo watu wengi.

Mwalimu wangu wa "Politics of Industrial States," alinifunza kitu kinaitwa. "How to read difficult passages."

Imenisaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni hatari sana ana ile story yake ya jemedari alliyekuwa ana pesa akaachana na kila kitu akaamua kuwa mtu safi na kumtumikia Mungu ila baadae anakuja hitimisha kuwa huwezi kuwa mtu mwema ukiwa duniani
 
Mimi nawapenda sana waandishi. Naona ni watu wenye akili sana na wengi hasa wale manguli huwa wananifurahisha kwa jinsi wanavyoweza kutumia kiswahisi ktk andishi zao. Huyu Bwana Mohamed Said ni mtu anaenivutia sana kiuandishi. Mara nyingine huwa sisomi kwa kuvutiwa na kile alichoandika bali ule mtiririko wake. Na tangu nianze kumsoma nimekua nimekua na uraibu wa andishi zake, huwa nasoma kila kitu na kiukweli huwa sitoki kapa maana mara nyingine kujifunza kitu pia ni kuamua. Kama wewe ni mtu wa kusoma huwezi kuacha kupenda au kuvutiwa kwa jinsi ya uandishi wa muandishi huyu. Hongera mkuu mimi ni shabiki wako kindakindaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jean-Paul Charles Aymard Sartre Mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchini Ufaransa aliwahi kuandika kumuhusu Ernesto "Che" Guevara, kwamba; “ not only an intellectual but also the most complete human being of our age.”

Ikiwa ni takribani miaka saba baada ya kifo cha Che.

Maneno haya ya muumini kindakindaki wa falsafa ya "Existentialism" bwana Jean-Paul Charles Aymard Sartre yanaungwa mkono na Andrew Sinclair mwandishi wa kitabu cha Guevara; kwamba ni kweli Che alikuwa 'Complete human being' katika hizo zama.

Katika umri wa miaka 39 tu Ernesto "Che" Guevara pekee yake alikuwa na 'career' nyingi pengine kuliko kundi lote la watu katika maisha yao yote.

[emoji1542] A doctor

[emoji1542] A diarist

[emoji1542] Political and military theorist

[emoji1542] A guerilla fighter

[emoji1542] An economist

[emoji1542]A tactician

[emoji1542] A banker

[emoji1542] A planner

[emoji1542] An industrialist

[emoji1542] An ambassador

[emoji1542] A propagandist

[emoji1542] And as the doer of all his other duties.

Sasa ni hivi, Tunafahamu Che alikaa darasani kusomea udaktari wa Binadamu;
Swali kujiuliza, ni lini tena Che alikaa darasani kusomea hizo 'career' zingine zote alizopata kuwa nazo?

Pichani ni Simone de Beauvoir, Jean-Paul Sartre akiwashiwa cha Arusha na Che Guevara walipokutana huko Cuba mwaka 1960.[emoji23]

Mshkaji wako,
Deusy Mwakalinga Jr.

COMMENTS ZA MOHAMED SAID

Deusy wewe mtoto hata sijui unatafuta nini kwangu.

Toka asubuhi mimi nilitambua mapema alfajir kuwa wewe ni mtu matata sana.

Jean Paul Sartre.

Che...

Mimi nakua mjini Dar es Salaam huyu Che na Malcolm X ndiyo walikuwa mashujaa wangu.

Umenikumbusha kwa kumtaja Jean Paul Sartre sheikh na mwalimu wangu Sayyid Omar Abdallah maarufu kwa jina la Mwinyi Baraka.

Katika miaka ya 1980 Muslim Student Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) walifanya seminar Nkrumah Hall na katika wazungumzaji alikuwa Mwinyi Baraka.

Ilikuwa si kawaida wasomi wa Kiislam kuzungunza Nkrumah Hall basi ukumbi ukajaa kuja kushangaa hawa nao wana nini?

Mwinyi Baraka akasimama kuzungumza hadi akamaliza.

Mwinyi Baraka ukimtazama kichwani ana kilemba, kizubao, kanzu na kashda begani.

Haikupitikii kuwa ni msomi wa University of Oxford.

Picha iliyowajia wengi pale ukumbini wasiomfahamu ni sheikh katoka Zanzibar.

Katika kipindi cha maswali na majibu akasimama kijana mmoja na ile ''body language,'' yake ikawa imejieleza yote.

Kwa kiburi na jeuri kijana akamwambia Sayyid Omar Abdallah kuwa dunia ya sasa ni dunia ya ''materialism,'' kijana akatamba sana pale.

Mwinyi Baraka kainamisha kichwa anamsikiliza kwa upole kabisa kijana akamfundisha sheikh, ''Theories of Development,'' kama zinzvyoelezwa na Marxists.

Kijana akamaliza.

Ukumbi ukalipuka, umechangamka, makofi yamepigwa kwa shangwe kama vile kusema, ''Hawa nini wanataka kutuletea mambo yao hapa yasiyokuwa na kichwa wala miguu."

Mwinyi Baraka akasimama kujibu.

Akatoa nukuu ghibu, yaani ''off head,'' ya ukurusa mzima wa Jean Paul Sartre kutoka sura ya kitabu chake kimoja anaisoma ile nukuu kwa Kifaransa.

Ukumbi umeanza kushtuka watu katika hadhira wanatazamana.

Kisha akamwambia yule kijana hayo uliyofundishwa hapa si mambo mapya Jean Paul Sartre alishayasema hayo miaka mingi huko nyuma.

Sheikh akasherehesha kwa kiasi chake.

Akahitimisha kwa kumwambia kijana kuwa mengine awaulize walimu wake ambao wako pale ukumbini watamfundisha.

Mwinyi Baraka akakaa kitako.

Nkrumah Hall ilikuwa kimya.

Ukiangusha sindano utasikia mlio wake.

Kijana aliyeuliza swali kwa kukosa adabu akawa mdogo kama ''piriton.''

Sent using Jamii Forums mobile app
Omar Abdallah ndiye aliyeandika "The Sage of Moroni?"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good and interested story...Mwandishi amekomaa Kiuandishi lakini cha kujifunza ni kwamba Kuna watu wanajua mambo na kwa undani zaidi na tusiwachukulie poa tukadhani shule zetu wao Hawajazipita.Waweza kumwona mtu kwenye career moja kubwe anazo careers zaidi ya hiyo uionayo na maranyingi ukimwona mtu anakuja chuoni kutoa mada basi ujue yuko vizuri upstair (Mwanazuooni).
 
Back
Top Bottom