Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JECHA NA NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR
Kuna mambo hayatokei kokote duniani ila Afrika na ukipenda unaweza ukasema Zanzibar.
Hebu fikiria kwa dakika moja tu mathalan Jecha kashinda uchaguzi wa rais na amekuwa rais wa Zanzibar.
Historia itamkumbukaje?
Unaweza ukajaribu kuingia ndani ya akili yake pia ukajiuliza hivi kimetokea nini kuifanya nafasi ya rais wa Zanzibar kuwa kitu cha kuchezewa ikaonekana kuwa nafasi ile ni chini mno kuwa yeyote yule anaweza kuiomba?
Unaweza ukajiuliza pia nafasi ya rais wa Zanzibar haina vigezo maalum?
Mbona nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ina vigezo vinavyofahamika vipi nafasi ya rais iwe wazi kwa Waingereza wanasema, "every Tom, Dick and Harry?
(Kwa lugha ya Kiswahili chukua majina matatu katika orodha ya wagombea urais katika orodha ya wagombea wa Zanzibar mfano Jecha na wenzake wawili ukayaweka).
Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar umekuwa kichekesho mfano wa circus.
Mgombea wa CCMZ anashindwa uchaguzi wa rais CCMZ inaandika barua Tume ya Uchaguzi kuwa hawakubaliani na matokeo vurugu inatokea kisha yule aliyeandika barua ya kukataa kushindwa anatangazwa mshindi (1995).
CCMZ inashindwa tena katika uchaguzi wa rais mwingine.
Kwa siku tatu Tume ya Uchaguzi inashindwa kutoa matokeo ya uchaguzi wa rais. Televisheni inaonyesha picha ya baadhi ya viongozi wa CCMZ wamejikusanya vikundi vidogo vidogo wamejiinamia kisha inatangazwa kuwa uchaguzi umefutwa (2015).
Wapi ulimwenguni mambo kama haya yanatokea?
Hivi kile kitabu cha Guiness Book of Records bado kipo?