Watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kufikiri matatizo ya Tanzania ni ya mtu mmoja badala ya system nzima ambayo ni mbovu na imeshindwa kutimiza majukumu yao. Hii ni tabia ya watu ambao wanashindwa kukubali part yao katika failures hizi mbalimbali na badala yake wanakimbilia kutafuta scapegoat.
Hata leo akifa RA ufisadi hautaisha Tanzania. Ni siasa za mufilisi kuamini kwamba nchi inayumba shauri ya mtu mmoja. Huyo RA hajaenda kuiba bank kwa mtutu au hajawafunga kamba viongozi wetu, amefanya anayofanya kwa kutumia watu ambao sisi wenyewe wengi wetu tukiwepo hapa JF tumewaweka serikalini pamoja na makosa yao mengi ya huko nyuma.
Miaka 20 iliyopita hakukuwa na ufisadi na bado nchi ilikuwa maskini pamoja na jitihada kubwa za watu kama Nyerere. Sasa badala ya kuelemisha jamii juu ya tufanye nini ili kuwasaidia wananchi wengi hasa wa vijijini ambao wanaishi kwa dhiki kubwa, kushuka kwa elimu, huduma mbovu za afya, mifuko iliyotoboka, sisi tunatumia zaidi ya 90% ya muda wetu kumjadili mtu mmoja tena with zero result.
Watu hao hao ambao kwa wakati mbalimbali walikuwa wakishirikiana na RA huku wakijua madudu yake, leo wanajifanya ni vinara wa kutuambia matatizo ya TZ ni RA.
Ili Tanzanzania iende mbele ni muhimu sisi sote nikiwemo mimi mtanzania, tujiangalie tena kwa kioo na kuona vipi tunaweza kubadilika na kutenda haki kwa watu wetu, kabla ya kummulika mtu mwingine kwa kioo hicho, tujimulike sisi kwanza. Tuna uwezo wa kubadili matendo yetu kabla ya kubadili matendo ya mtu mwingine.
Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?
RA tumemtengeneza wenyewe shauri ya tamaa zetu za haraka haraka na kufikiri maisha bora yanakuja kwa ujambazi. Kuamua kusaliti mamilioni ya wananchi waliotupa nafasi ili tujilundikie mapema na kuishi kama tuko ahera. Leo sisi Watanzania wote tukiamua kutimiza wajibu wetu, hao akina RA hawatakuwepo.
Ni nani mbunge wa CCM ambaye anaweza kuapa kwa mungu kwamba hakufaidika na mapesa yaliyooza ya Rostam na genge lake? Mtu akisema hivyo atakuwa anadanganya tu kama wanavyodanganya kwenye mambo mengi.
Ndio maana watu wengine tumepunguza kuchangia JF kwasababu mwelekeo sasa umeanza kuwa mtu badala ya system au fikra. Tumeanza kugeuza fikra zetu na kuanza kuwa mimi na yule au sisi na wale. Tunajaribu kwa nguvu zote bila mafanikio kuingiza pumba kwenye vichwa vya Watanzania ili waweze kuamini kwamba tatizo letu ni mtu mmoja.
Binafsi naamini mawazo kama haya hayamsaidii mtu yeyote na badala yake yanazidi tu kuligawa taifa. Lazima tutengeneze principles ambazo tuko tayari kuzisimamia na kuzilinda bila kujali aliyekiukwa na RA au Mengi. Vinginevyo na sisi wengine tunageuka kuwa vikaragosi vya hawa wababe ambao wameitumia system kufika pale walipofika na sasa wameamua kugeukana.