Mkuu, nisaidie kidogo hapo. Hao wakuu wawili hapo waligombea na kushinda viti gani?
FMES,
Nasikia na Wassira naye alipewa millioni 2 na RA alipogombea kule Bunda. Ni nani miongoni mwa mawaziri wa sasa ambaye hakupata mshiko wa RA?[/QUOTE]
- Dawa ni kuwafunua tu hapa, hakuna kulala!
FMES!
Gademu!!! this is what I call "case closed" kwani imejibu maswali karibu saba yaliyokuwa yananitatiza!! Thanks mkuu.. Mengine nakutumia kwenye PM.. maana ni too hot..
HUU NDIYO 'UKONDOO NA OWOGA' badala ya kutuandikia hapo enaeema its too hot. kwa uwoga wako unogoka kuandika je unaweza kuwa na uwezo kusimmama na kueleza baya la mtu, unaopa nini, halafu unajifanya wewe ni mkosoa mabaya katika jamii, hovyo kABISA
yaani wewe nimekuwa HUFAIII KABISA KATIKA JAMII, huna tofauti na JITU PATEL au HITLER enzi hizo
wewe unaye faa katika jamii yepi uliyo kwisha ifanyia hiyo jamii?
Ndugu wana JF,
Nina amini kabisa kwamba Watanzania tuna shughuli nyingi na muhimu sana kwa ajili ya ujenzi wa Taifa. Maada hii kwa upande wangu ninaiona imejaa majungu,fitina na uzandiki.
Quote: Kidatu
Jambo langu la mwisho nilikuwa naomba kuuliza nini maana na neno FISADI?
Quote:- Kidatu
Re: Shule ya NIMROD MKONO
Mkono pamoja na kwamba ni fisadi lakini anakumbuka nyumbani. Sehemu ya Pesa anayopata anaitumia kujenga mashule na zahanati mkoani kwake. Shule ambayo anajenga sasa inakadiriwa kuwa na gharama za $1.6m na watoto wanakwenda shule bure ama kwa gharama kidogo sana.
Ndugu wana JF,
Ninasema hivyo kwa sababu wachangiaji wengi katika mada hii wamekuwa wakitaja majina ya nani alipewa nini ama alisaidiwa nini na Rostam Aziz ili kuwa hapo alipokuwa leo, bila ya kuleta ushaidi wa kauli zao. Unakurupuka na kusema fulani alipewa pesa na Rostam na mpaka kiasi cha pesa unakitaja, sasa kwanini usilete na ushahidi kamili wa kile unachokisema?.
Tuwe makini katika yale tuyasemayo ama tuandikayo, si vyema wala si busara kumshuhudia uwongo mtu mwingine. Kama huna ushahidi ama huna hakika ni bora kukaa kimya bila ya kuchangia mada husika.
Quote:- Kidatu
Re: Shule ya NIMROD MKONO
Mkono pamoja na kwamba ni fisadi
Nadhani jina sahihi la huyo mwenyekiti wa CCM dodoma ni William Kusila!1. Abdulaziz - Ubunge Lindi. 2. Mongella - Ujumbe NEC na UV-CCM.
2. - Mkulu Mwanakijiji ongeza kwenye kundi A:-
Wilson Kusila alipewa Millioni 15 na Rostam, na kushinda Uenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma alionao sasa Mwaka 2007.
FMES
Nadhani jina sahihi la huyo mwenyekiti wa CCM dodoma ni William Kusila!
Au tuseme nchi hii ina Rais (aliye Ikulu) na pia ina Mgawa Madaraka a.k.a King-maker a.k.a RA a.k.a untouchable?
Kaka nakujua toka siku nyingi kuwa wewe ni ndugu kibaraka wa Seguyemisi kwa muda mrefu na kweli unajua nyeti nyingi za kweli na za uongo za ccm na hii inatokana na kokaa jikoni na Miss Anne Killango mara kwa mara....lakini kinachonishangaa ni kuwa you had never stopped dreaming about Nchimbi.Huwezi kaa mwezi bila kumtaja........aliwafanya nini kwenye huo ukoo wenu wa Seguyemisi?sambusa?hahahahahahaha au uraiswa embe bivu hahahahahah au aliwaloga hahahhahahahahaah.kweli jamaaa kiboko ya ukoo wenu1.
2.
- Haya anza wewe kwanza kuleta ushahidi wa ufisadi wa Mkono mkuu!, Tunajua kwenye huu msafara wa mamba hata makenge mmo, najua umechukia kwa sababu rafiki yetu Nchimbi ametajwa, pole sana hapa ni mwendo wa mdundo tu, sasa lete ushahidi wa ufisadi wa Mkono?
- On my part Ndejembi na Kusila, walimshinda mshikaji wangu wa karibu sana Bwana Masima, je inaweza kukusaidia kujua kwamba I have an-idea na ninachokisema mpaka the amount na hata waliopewa?
- Sasa think again nani anayetakiwa kunyamaza hapa bwa! ha! acha kurukia treni kwa mbele mkuu maana ni hatari!
Respect!
FMES!
Kaka nakujua toka siku nyingi kuwa wewe ni ndugu kibaraka wa Seguyemisi kwa muda mrefu na kweli unajua nyeti nyingi za kweli na za uongo za ccm na hii inatokana na kokaa jikoni na Miss Anne Killango mara kwa mara....lakini kinachonishangaa ni kuwa you had never stopped dreaming about Nchimbi.Huwezi kaa mwezi bila kumtaja........aliwafanya nini kwenye huo ukoo wenu wa Seguyemisi?sambusa?hahahahahahaha au uraiswa embe bivu hahahahahah au aliwaloga hahahhahahahahaah.kweli jamaaa kiboko ya ukoo wenu
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku ilipowasilisha taarifa yake kwako, Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo ya ziada ya mradi huu nitayatoa baadaye.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.
Mheshimiwa Spika, leo tunapowasilisha taarifa hii mbele ya Bunge lako tukufu, tunajisikia kuutua mzigo mzito sana ulioanza kutuelemea kutokana na kuzongwa kila kukicha na kila aina ya uzushi, uchochezi, uchonganishi na hata vitisho. Tumezushiwa kuhongwa magari ya kifahari na fedha taslimu; tumetuhumiwa kuendesha vita dhidi ya Waislamu na mara nyingine tuhuma hiyo ikageuka kuwa vita dhidi ya Wakristo ndani ya Serikali; tumesingiziwa kuibadilisha taarifa yetu mara mbili, baadhi wakisema kwa ushawishi wa fedha, wengine wakidai kwa shinikizo la Mhe. Spika na wengine kwa shinikizo la Waziri Mkuu; tumeshuhudia pilikapilika za usiku na mchana za kujipanga na kuwashawishi baadhi ya Mawaziri na Wabunge kuikana taarifa hii na mapendekezo yake kiasi cha wengine wetu kujiuliza: kulikoni mtu asiye na hatia kuweweseka?
Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati Teule, kukuhakikishia wewe binafsi na Bunge lako tukufu kuwa tumekamilisha kazi tuliyopewa kwa uaminifu na ujasiri mkubwa, dhamira safi, moyo wa uzalendo na kwa kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu katika kila tulilolifanya. Tulichukua kila tahadhari tusibanwe na mgongano wowote wa kimaslahi kiasi kwamba mjumbe mwenzetu, Mhe. Eng. Stella Manyanya, mwajiriwa wa muda mrefu wa TANESCO ambaye alikuwa kwenye likizo isiyo na malipo, akaamua kukatisha ajira yake kwa kujiuzuru. Aidha, tunakuhakikishia Mheshimiwa Spika kuwa hatukupokea senti tano ya mtu wala baiskeli yake. Mwenye ushahidi tofauti, basi alithibitishie Bunge hili tukufu. Mimi na wajumbe wenzangu wa Kamati Teule tuko tayari kuwajibika kisiasa.
M Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.
Fisadi Mtoto
Re: Jedwali la RA: Nani hayumo?
Hio ripoti watu wenye akili hatuiheshimu tena ilijaaghiliba majungu na fitna ambazo zinaendelea mpaka leo