Jee huku ni kutokufahamu ama ni Makusudi?

Jee huku ni kutokufahamu ama ni Makusudi?

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
jaji-rama.jpg


Jaji Agostino Ramadhani

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Agostino Ramadhani akizungumzia mwelekeo wa utoaji maoni kuhusu Katiba Mpya unavyoendelea Zanzibar amekaririwa na gazeti la ZANZIBAR LEO akisema "anashangazwa na wengi wanaopewa nafasi ya kutoa maoni yao katika mchakato huo wamekuwa wakizungumzia zaidi mfumo wa Muungano wakati kukiwa na maeneo mengi ambayo wananchi wa Zanzibar wanaweza kuyatumia kama sehemu ya kuainisha mahitaji yao katika misingi ya katiba mpya.

Akiyataja maeneo hayo alisema kuna masuala ya ardhi na kero za wawekezaji kwa kuielekeza serikali namna ya kuzifanyia kazi kwa misingi ya Katiba kutokana na hivi sasa bado wananchi wamekuwa wakilipigia kelele eneo hilo."

Najiuliza hivi Jaji Ramadhani ambaye ni mwanasheria aliyefikia nafasi ya kuwa Jaji Mkuu hajui kuwa maeneo ya ardhi na kero za wawekezaji hayamo katika masuala ya Muungano na katika maeneo hayo Wazanzibari wanatawaliwa na Katiba ya Zanzibar na siyo Katiba ya Muungano?

Vipi alitegemea Wazanzibari watoe maoni kuhusu mambo hayo kupitia mjadala wa Katiba ya Muungano?

Kioja kama hiki alikizua Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (na huyu naye ni mwanasheria na Jaji) pale alipokwenda kufuatilia utoaji wa maoni kisiwani Pemba akasema anashangaa alikuwepo Tanga na wananchi wakawa wanatoa maoni kuhusu elimu na walimu, lakini Pemba hawazungumzii hayo na badala yake wanazungumzia Muungano tu. Alitushangaza maana kwa mtu wa hadhi na elimu yake alipaswa kujua kujua kuwa elimu na walimu si mambo ya Muungano.

Kinachoonekana ni kuwa maoni ya Wazanzibari kuhusu Muungano yanawatia kiwewe Joseph Warioba na Agostino Ramadhani. Wanachopaswa kukifahamu ni kwamba katika suala la Muungano, Wazanzibari hawatarudi nyuma katika kusimamia wanachokiamini.

Ni vyema Warioba na Agostino wakapata nafasi ya kumsikiliza Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Karume, hotuba yake ya Kizota ili wapate darasa la uvumilivu kwa wenye mawazo tofauti na yao na waache kuwapotosha Wazanzibari kwa kuwataka watoe maoni kwa mambo yasiyowahusu kwenye Katiba ya Muungano.
 
Back
Top Bottom