Jee ushawahi fikiria njee ya Boksi??

TOHATO

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2016
Posts
1,336
Reaction score
4,653
Neno umefungwa haimanishi upo gerezani ila Ni jinsi gani fikra zako hazitoki njee ya (unayoyaamini) kutokana na sababu flani. Sababu hizo hueza pelekea kuwa mshabiki pekee bila kuhoji au kuhitaji kudadisi zaidi ya hapo.

Kuwa ndani ya Boksi kunaeza kukawa ni DINI SIASA, au hata SAYANSI.

Ni vipi MTU huwa ndani ya boksi?
Je waelewa upo ndani ya boksi?

MFANO
Ukitaka jua umo ndani ya Boksi angalia inapotolewa mada ya DINI wewe unatetea wapi? Je ushajiuliza kwanini watetea hapo tuu? Unaeza jipa moyo kwa kusema kwa vile ndo sehem sahihi,jee huo usahihi umeufikiria ukiwa njee ya boksi?
Karibia wote Dini tumezikuta toka kwa wazazi hali ilotupelekea kuwa ndani ya Boksi. Na Siku zote DINI hukufanya kuiamini bila kuhoji huku ikiiponda dini nyingine( hapa boksi ndo linapoanzia)
. Ni ngumu kusema ipi ndo Dini sahihi huku ukiwa ndani ya Boksi.

Hata kwenye siasa ,wapo ambao hupenda upande flani(Vyama). Hata kama ataona ubovu mkubwa ndani ya chama chake atatumia njia ya kutetea ili kuufrahisha moyo wake. Ni ngumu kujua mengi kama utasoma gazeti LA (Uhuru,Tanzanite) au kuiskiza TBc kama wewe ni ccm Au kusoma gazeti la Tanzania Daima kama wewe ni mpinzani.

Njia pekee ya kutoka njee ya Boksi ni kwa kusoma vitabu bila upendeleo na ushabiki
 
Kufikiri nje ya sanduku sio kama mtu anavyoweza kudhani, wala sio tu kutafakari kwa mwangaza wa akili.

Kuacha eneo lako la faraja la kisaikolojia na kuchunguza "ufumbuzi katika ulimwengu usiojulikana nje na hii huhitaji hatua kubwa za mwongozo wa akili, ujasiri, na → ubunifu -

Pia pata mwongozo wa msukumo kutoka kwa mtu au kitu ambacho kimetoa mwelekeo au kwanini ufikirie zaidi au mtu ambaye huanza kutoa mawazo yatakayokufanya uanze kujiuliza ni wapi nimetoka,,au ni wapi ninaenda na nini hatima ya mwisho wa haya niyawazayo..??


Ni ngumu sana kwa mtu ambaye kawa mfia dini wa jambo flani au mapokeo flani ambayo kayakuta kutoka kizazi kilichotangulia kwake kwa kuyaishi na kuendelea kuyasikia..

Mara nyingi inakuwa ngumu kutoka kwenye mstari make pre existing life style zinatukosti snaa...

mara nyingi jambo linalofanywa na watu wengi au jambo linaloaminiwa na watu wengi ndo hubeba msingi wa ukweli kama tunavyodhani na kila kizazi kinachokuja huyapokea bila kudigest( bila kufikiria) na matokeo yake kama ni sumu huweza kuenea sehemu yote lakini inapaswa kujenga mazoea ya kujitoa ufahamu na kufikiri njee ya ukweli huo..

mara nyingi jambo linaloaminiwa na wengi huwa lina siri nzito sana kwa watu wachache...

Think outside will make you understand how truth inside the reality is..

Kuna mambo mengi sna ambayo hatujui hatima yake kutokana na kuaminishwa mambo mengi sna..

Mambo kama dini,imani ,uwepo wa viumbe kutoka nje ya sayari yetu yamekuwa ni mambo yanayobeba nafsi kubwa sana katika maisha yetu na kufanya kundi kubwa la watu kuwa na imani tofauti ..

Lakini ili upate ukweli wa juu ya haya inakupaaa ufikirie njee ya maneno au mapokeo uliyoyakuta pengine unaweza pata jibu sahihi..

wakati mwingine unapaswa ujitoe kafara kujua ukweli..

Mind you that,Reality is synchronized with the risk...

Ukitaka kujua ukweli jitoe kafara nje ya mstari wa ukweli ukioukuta




Sent using Jamii Forums mobile app
 
i like this comment bro.
 
Hekoo mkuu Hekoo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…