Jeep® nao watoa first EV: Jeep Wagoneer S

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Hakuna jinsi.

Kampuni la Kimarekani Jeep nao wamedandia treni, ingawa kwa kuchelewa kidogo, na kutoa first EV, Jeep Wagoneer S.

Hii ni large SUV itakayokua na 600 hp kutoka kwenye electrical motors mbili, na batteryla 100kWh lenye uwezo wa kutembea kilometa 480 ikiwa full charge na utaweza kulicharge kutoka 20% to 80% kwa dakika 23 tu ukitumia DC fast charging (Level 3). Kwa Level 2 charger utatoka 5% to 80% kwa masaa 7 na kwa Level 1 chargwr utatumia masaa 53 kutoka 5% to 80%.


Kwa mbele haijautupa muonekano wa "Jeep" kua na matobo 7 pale mbele kwenye grille.

Kwa ndani, hii gari yenye siti 5 ina screen kubwa ya inch 45 pale mbele na mazaga zaga mengine kama unavyoona.


Kwa maelezo ya Jeep, itauzwa kuanzia $72,000.
 
Kitu ambacho kinanishangaza kwenye magari ya UMEME ni bei zake Tu za kutupa nashindwa kuelewa kwanini yanauzwa bei rahisi Sana,
Fikiria hiyo gari ikija huku kwetu kama used itauzwa kiasi gani au yale magari ya kichina yanayouzwa $32,000 baadae yakija huku Africa nahisi yatakuwa kama bei ya pikipiki tu
 
Almost 1/2 ya bei uwa inashuka miaka 2 ya mwanzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…