Jeetu Patel karudi...

miracles hazitokei tena duniani kote isipokuwa tanzania.

hapo kunapikwa jungu kubwa kweli kweli, wananchi tutaambiwa Pesa ZOTE zimerudishwa (bila ya ushahidi wowote), tutaambiwa hao watu wamezuiliwa kupewa msaada wowote kutoka serikalini kwenye biashara zao (kama ADHABU), na huo ndio utakuwa mwisho wake.

tusubiri kuibua ufisadi mwengine, tushangirie kwa siku mbili tatu, ila kwa kufikishwa mahakamani kina rostam aziz, BADO, nasema tena BADO!
 

Hypothesis
 
Mtoto

Kila kitu kinawezekana Tanzania, siwezi shangaa kabisa jamaa wakipata free lunch...and ride

Si unaona Dito pamoja na kuuwa kwa makusudi anapeta tu na biashara za asali nasikia hutumia gari la serikali vile vile...hii ipo Tanzania tu

Mwana mi pia naunga mkono, kwa TZ kila kitu chawezekana, kuna wakati mtu alitolewa wadawa ya kulevya tumboni mkemia mkuu kapewa sample kasema simenti!!!!! BONGO.
 
mmhhh! basi ameogopa! manake yumo kwenye interpol wanted list!
 
Mbwa ni rafiki mzuri wa binadamu ila usikanyage mkia wake!
 
Mwana mi pia naunga mkono, kwa TZ kila kitu chawezekana, kuna wakati mtu alitolewa wadawa ya kulevya tumboni mkemia mkuu kapewa sample kasema simenti!!!!! BONGO.
Whaat? hivi mwizi ukiiba ukijulikana ukirudisha ulichoiba ndio basi hamna hata kesi ni msamaha tuu? Hivi seria ya wahujumu uchumi inasema je? na kuhusu wizi sheria nayo inasema je?

Hii ni made in Tanzania
 
Tanzania Daima

SERIKALI itaweka hadharani kiwango cha fedha kilichorudishwa na kampuni zilizochota fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), baada ya wiki mbili kuanzia sasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mustafa Mkulo, alipozungumza na wakurugenzi watendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) waliopo nchini.

Wadau hao walikuwa wakizungumzia changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye juhudi za kuleta maendeleo pamoja na matumizi ya fedha za misaada za IMF.

Mkulo alisema serikali itataja kiasi hicho na fedha pamoja na akaunti zao, lakini haitakuwa tayari kutaja majina ya watu hao kwa sababu ambazo hakuziweka bayana.

“Najua watu wana hamu ya kutaka kujua kiasi cha fedha kilichorejeshwa na kinachoendelea kurejeshwa, lakini kwa sasa ni mapema mno kufanya hivyo ila nina ahidi tutatangaza kiwango na akaunti namba baada ya wiki mbili zijazo kuanzia leo (jana),” alisema Mkulo.

Alisema serikali haina cha kuficha inapofika katika suala la ubadhirifu wa mali za umma na ndiyo maana wahisani na IMF wameridhika na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu waliohusika na upotevu wa fedha za wavuja jasho.

“Serikali tumekuwa wazi katika kushughulikia tuhuma mbalimbali na pia tumekuwa tukiwawajibisha watu wanaohusika na tuhuma hizo, ndiyo maana wenzetu hawa wa IMF wametuelewa na kutuunga mkono katika juhudi zetu za kupambana na watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi,” alisema waziri huyo.

Naye Mkurugenzi wa IMF kutoka nchini Ufaransa, Jonathan Fried, alisema IMF imeridhishwa na hatua za serikali zilizochukuliwa dhidi ya watu wanaotumia vibaya rasilimali za nchi, hivyo kuchelewesha maendeleo ya taifa.

“Tumeridhishwa na Serikali ya Tanzania ilivyolishughulikia suala la EPA, na sisi tutaendelea kuisaidia, ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika kujikwamua kiuchumi,” alisema Fried.

Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali nchini wameitaka IMF kufanya mapinduzi ya sera zake, ili kuweka masharti ya misaada kwa nchi maskini kulingana na uwezo wa nchi hizo badala ya kuweka masharti ya jumla kwa nchi zote.

Profesa Hamphery Moshi, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema masharti yasiyozingatia uwezo wa nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia nchi zenye uchumi mdogo kutoendelea kiuchumi.

“Kuna haja kwa nyinyi wataalamu wa IMF kufanya mapinduzi katika sera zenu, ili masharti ya misaada yaendane na uwezo wa nchi, tofauti na ilivyo sasa ambapo masharti yote ni sawa,” alisema Profesa Moshi.

Hussein Kamoto, kutoka Shirikisho la Wafanyabiashara wenye Viwanda Tanzania (CTI), alisema kutokuwapo kwa miundombinu imara na kupanda kwa bei ya umeme kila mara ni miongoni mwa sababu zinazochangia Tanzania kutopiga kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa muda uliokusudiwa.

Alisema gharama za uzalishaji wa hapa nchini zimekuwa juu kutokana na matatizo hayo, hivyo ni vema wataalamu hao wa IMF wakaangalia zaidi maeneo hayo, ili kuweza kuisaidia Tanzania.

“Uchumi wetu hauwezi kuendelea katika mazingira haya tuliyonayo ya gharama kubwa za umeme pamoja na miundombinu mibovu, hivyo ni jukumu lenu nyinyi wataalamu kumshauri mkuu wenu atusaidie kulingana na hali ya mambo mlivyoiona,” alisema Kamoto.

Naye Ali Mufuruki, alisema Tanzania ielekee katika kujitegemea zaidi badala ya kutegemea misaada ya IMF na wahisani wengine, ambayo wakati mwingine ina masharti magumu na yasiyoendana na matakwa ya nchi.

Profesa Idris Kikula, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, alisema ili Tanzania iweze kuwa na dira nzuri ya kuelekea katika maendeleo ni lazima iongeze idadi ya kudahili wanafunzi wa elimu ya juu.

Alisema Tanzania inadahili wanafunzi wachache zaidi katika ukanda wa Afrika, hivyo ni vema juhudi za makusudi zikatumika kuboresha sekta ya elimu ili nchi iweze kuwa na wataalamu wa kutosha watakaokuwa na uwezo wa kupanga mipango itakayoliwezesha taifa kujitegemea.

Wataalamu wa IMF wapo nchini kujadiliana na wadau mbalimbali kuangalia ni maeneo gani yapewe kipaumbele katika misaada inayotolewa na shirika hilo nchini.

Mbali na waatalamu hao kuwapo hapa nchini, pia mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo anatarajia kuwasili nchini leo, kwa lengo la kuangalia namna ya kuongeza misaada kwa Tanzania na maeneo ya kuyapa kipaumbele.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Miundombinu, Adrew Chenge, Gavana wa BoT, Professa Beno Ndullu na maofisa mbalimbali wa serikali.

My Take:

Napiga muluzi!
 
Sasa this can divide the country big time, Yaani hili linaweza kuingiza Tanzania kwenye ditch. If Mkulo believes kwamba Watanzania doesn't diserv kujua ni nani aliyerushidisha, it is the same as kututukana matusi ya nguoni.

Mkulo is elected official whose salary relied on our taxes. Where is Upinzani guyz, where are they? That is red flag, Mkulo alisema serikali itataja kiasi hicho na fedha pamoja na akaunti zao, lakini haitakuwa tayari kutaja majina ya watu hao kwa sababu ambazo hakuziweka bayana.

Now kama wewe ni mpinzani that is a soar eye, you keep punch it. Yaani hapo ndio mahala muafaka pa kuitisha maandamano, hapo ndio mahala muhumu pa kuongea na International media.

Mwanakijiji, please help me! Where is upinzani? Yaani huyu Mkulo (Mr Fake MBA) anakuja madarakani na kutuambia tax payer what he will do? Is he out of his mind?
 
Hypothesis

Dar es Salaam
Mengi yalianzia hapa,kama utakuwa mtanzania mwenye akili timamu,BOT,Buzwagi,Richmond contract kuvunja kwake kulianzia hapa. wasioamini na waliosikia wakasema,hawashughuliki na mambo ya kwenye internet na hypothesis za watu.Mwisho wa siku ikawaje?
Tunasubiri hatua zipi zitachukuliwa kwa wale wanaodaiwa walichukua hizo fedha,kwani kuna moja anadaiwa Bilioni 16 alizochukua kwa kutumia nyaraka za kughushi aliweka kwenye fixed account,hivyo atazirudisha. Tunasubiri kuona,kama tunavyoona ya Mahalu
 
Huyu Mkullo nae ni Mmojawapo.

Kama walikua tayari kutaja makampuni na majina ya wamiliki wa hayo makampuni, Je iweje Leo katika kurudisha walichoiba iwe siri? Hii inamaana walioiba sio waliotaja ndio maana wanaona aibu kuweka majina yao hazani kwani na la mkullo lipo pia so anataka kujiwekea pazia.

Pili, kama mtu alipewa pesa arudishe pesa kiasi alichochukua na riba. So suala la serikali kutaifisha nyumba au majengo ya watuhumiwa sio sahihi bali ni kuziuza kwa njia ya mnada ili kupata fedha zilizoibiwa(kama ilivyo kwenye mikopo). Na hizo nyumba tutajiwe majina ya walionunua na kiasi alichonunulia na zisiuzwe chini ya thamani ya ununuzi.

Tatu, Nashindwa kujua Polisi (IGP, DCI)ambao wapo kwenye hiyo kama kwa kushindwa hata kuwashitaki hawa mabwana japo kwa kosa la Kufanya forgery na kosa la wizi wa kuaminiwa(COMPANY FAKE,claims document fake) wakati wanashughulikia hayo makosa mengine haya yako wazi na kitendo cha kurudisha fedha tayari ni ushahidi tosha waliidanganya na kuibia bank.

Kweli Ufisadi hautaisha maana IGP, DCI,et al wanatarajia na wao kujenga kapalace kutokana na EPA
 
Mimi naona hapo tunafungwa bao lingine, mbona wanaoiba kuku hawaambiwi warudishe kuku na yaishe? Hii ni kama janja ya kuwasaidia marafiki zao kama akina Rostam.
 
Mimi naona hapo tunafungwa bao lingine, mbona wanaoiba kuku hawaambiwi warudishe kuku na yaishe? Hii ni kama janja ya kuwasaidia marafiki zao kama akina Rostam.

Na ndiyo maana hawataki kuwataja majina. Sasa unaposema tutatoa amount na account number without majinaz hapo unakuwa unafanya nini kama siyo usanii?

Nadhani tatizo lililopo ni kwamba hizo hela zilipitia kwenye hizo kampuni fake na kuishia kwenye account za watu binafsi ambao wako serikalini ama wana uhusiano wa karibu na watu wa serikalini na hivyo kuanza kuwataja majina ni sawa na kuiumbua serikali. Hapo ndo tumeishaliwa tayari na kwa mwendo huu ufisadi hauwezi kuisha.

Halafu watu wanamshangaa Prof. Mwandosya anaposema mawaziri wanaochelewa kulipa bill za maji majina yapelekwe kwake badala ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari. Kumbe wamejifunza au labda ni fashion ya baraza jipya la mawaziri wasiumbuane mbele ya wapiga kura wao!
 

This guy mimi naye ni personal tu na anajua hili na mimi najua hili, hata kama Kikwete akimwachia (maana inaonyesha kwa Kikwete ana mpango wa kusamehe mafisadi wote kuanzia huyu hadi maregesi) lakini hapa halali mtu hadi kieleweke.
 


Safi saana bwana....ila hawa jamaa ilibidi kama tunavyosema "uji na mgonjwa uwezi kuviachanisha" na wao tunasema " mafisadi na segerea uwezi kuviachanisha",...hata kama wamerudisha...kumbuka mwizi uwa haachi tabia ya udokozi...

Mimi nasema lazima waende segerea....kwani iliwekwa kwa ajili ya nani?? Ebu niambie..😕[/
COLOR]
 
Nina mpango wa kuiba hela serikalini halafu nizizungushe weee! baada ya kupata faida nirudishe mtaji wao kwa mbwembwe. Nani mwenye dili jamani nikaibe serikali? Si nitarudisha tu bwana nikishtukiwa, kwani kuna noma!

Na nitahakikisha nakwapua hela nyingi sana, otherwise nikiiba vihela mbuzi waswahili wanaweza kunichoma moto ati. nitaiba midola mie!
 
Katika Taifa hili la Wadanganyika sidhani kama kutakuja tokea jipya labda karne ya 25. Nimetazama matokeo mengi ya uchaguzi mdogo tena yote yakiwa katika scandal kubwa kubwa (Mfano ile ya Buzwagi na hii ya BoT) lakini ndio kwanza CCM wamejizolea kura..Na sababu kubwa ni kwamba CCM wanafahamu kumwongoza kipofu kwa fimbo yake sio maneno, ishara,darasa ama maelekezo ambayo hutumiwa na vyama vya Upinzani. Wadanganyika sii wajinga nadhani wengi wetu vipofu wa akili (haioni mbali zaidi ya marefu ya mkono).

Kifupi, Ukitaka kupata mafanikio TZ basi usije akifikiria nje ya mfumo mpya wa Chumuka Chako Mapema laa sivyo basi upo karne moja nyuma ama enzi za Ujamaa. Naanza kuamini kuwa ukipewa madaraka, mshiko, panga nchini Tanzania basi ni Ujuha kama hutaitumia nafasi hiyo kujitajirisha.
Potelea mbali maslahi ya Taifa, hayo yatajengwa na kizazi kijacho mwaka 2500. Inauma sana lakini ndio reality!
 

Mkandara hii statement ingawa ni ya uchungu lakini ina ukweli. Umeona mapokezi ya kishujaa kule kwenye jimbo la Lowasa na kile ambacho ameanza kufanya na mafisadi wenzake kina Karamagi ambao wana ccm wanawaita mashujaa kwa walichofanya!?
 
WATZ tunafanywa watoto wadogo na tunaburuzwa na tuliowaweka wenyewe madarakani,hapa kuna siri kubwa sana ambayo ipo na watanzania wameshafunguka macho,haya mambo yote yanayosemwa ni viini macho kwa watz kwa kuwa serikali inatambua mwamko wa wananchi kutaka kujua upo juu,nawaambia ndg zangu kuwa hili suala ndio linamalizwa kiaina,kwani hizo pesa za EPA ndizo zilizoiingiza CCM madarakani,NANI MWENYE UBAVU WA KUWABURUZA MAHAKAMAI?
 
Mwafrika wa Kike,
Mkandara hii statement ingawa ni ya uchungu lakini ina ukweli. Umeona mapokezi ya kishujaa kule kwenye jimbo la Lowasa na kile ambacho ameanza kufanya na mafisadi wenzake kina Karamagi ambao wana ccm wanawaita mashujaa kwa walichofanya!?

Sina la kuongezea, yote haya yamenivuruga kabisa akili... kisha nikakumbuka usemi wangu ule wa zamani ambao kule Bcstimes nilipigwa vita vikali sana... Nilisema hivi sisi watu weusi ni manyani tu! tofauti kati yetu, wapo wale wanaocheza sarakasi wakivaa suti nzito (white color) na wengine ndio tupo porini na mashambani kuvizia mazao (walalahoi), lakini sote hatuna tofauti, sote manyani makalio yetu pekee ndio mekundi au pink.... na pengine labda sayansi inaweza dhihirisha kuwa sisi ndio tupo ktk stage ya mwisho kuingia Ubinadamu...
Mtanisamehe sana na nakuombeni radhi pamoja na haya yote kwani inaniuma sana. Labda matusi kidogo yanaweza kuwaamsha Wadanganyika maanake nimeambiwa ukitaka kumwasha mtu mweusi mtukane ama mtukanie mama yake, hasira na machungu yatakubali vizuri na mizimu ya babu zake itapanda kuliko uchungu wa nchi yake!..

Sioni nje kabisa!.. tumekwishaaaa!
 
Damn, Yaani wanarudi na kutuchezea kwamba wanarudisha pesa waliyokuwa wameikwapua? Mbona wezi wa kuku wanaishia Keko? Sasa hao TAKUKURU na sijui Police wako wapi? Wanaishia kuwapiga bakora wapiga kura wa Kiteto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…