Rohombaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 13,067
- 10,393
Mahakama ya wilaya ya Kinondoni leo imemuhukumu mwanamke mmoja mkazi wa Tandale Imelda Elisha (28) kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la wizi.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Joel Mwambuta amesema amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la wizi wa kuaminiwa baada ya kusikiliza mashahidi 3, pamoja na vielelezo ikiwemo risiti ya miamala iliyowakilishwa na Samsoni Mshana ambaye ndiyo mlalamikaji.
Akisoma hukumu hiyo bila ya kuwepo mshtakiwa ambaye ameruka dhamana ameagiza adhabu yake ianze mara tu atakapokamatwa na wakati huohuo amemuamuru mshtakiwa kulipa kiasi cha Shs 103,000/- kwa mlalamikaji.
Inadaiwa Septemba 22, 2019 mshtakiwa alipokea kiasi hicho cha pesa kutoka kwa mlalamikaji kama nauli ya kutoka Dodoma kuja Dar na hakwenda Dar Kama walivyokubaliana na wala hakurudisha fedha hizo na wala hakutoa maelezo yakuridhisha.
Sent using Beretta ARX 160