Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Imefika wakati wa kupima ubora wa elimu yetu kwa kuangalia idadi ya watu wanaokutwa na hatia na kwenda jela. Idadi ya wafungwa na magereza yanatosha kutuonyesha tuna ubora wa elimu kiasi gani.
Ikumbukwe kuwa matukio ya kihalifu kama rushwa, wizi, utapeli, nk. Ni matokeo ya elimu inayowaonyesha wanafunzi kuwa ‘material gain’ ndio kitu cha kwanza katika maisha yao, pesa kabla ya utu. Matukio haya yamewapeleka vijana wetu wasio na ajira jela kwa matukio ya wizi nk. Wengine waliokuwa kwenye ajira wamejikuta jela kutokana na rushwa walizokuwa wanazihitaji ili kuongeza kwenye mishahara yao na kuishi maisha ambayo waliyatamani wakiwa shuleni.
Wale vijana ambao hawakutumia muda mwingi shuleni kwa kuacha shule au kutofika kwa ukosefu wa ada ndio wamekuwa vibaka, wakike wamekuwa Malaya. Na pia kwa kuwa elimu imejaza mashindano katika nafsi zao, wale ambao jamii inawaambia wameshindwa wamejikuta wakajawa na chuki kiasi cha kufanya matukio ya kikatili hata kwa mambo madogo madogo kabisa. Mambo ambayo yanatosha kupuuzwa, hawa vijana wenye chuki yaliwapeleka jela kwa kuwa walitiana ngeu au kuuana kabisa.
Nasema ubora wa elimu unaweza kupimwa kwa kuangalia matukio haya, kwa kuwa kama shule itamfundisha mtu kufikiri, kuwa kwa ajili ya jamii yake, hata akiacha shule fikra zitamsadia kuishi na watu wa jamii yake. Matukio ya kihalifu yatapungua kwa kuwa mtu atakuwa anafanya vitu kwa ajili ya watu wake na sio kwa ajili yake binafsi tu.
Elimu bora ni ile inayofanya, wachache waliosoma kutosha kuhudumia jamii yao, na kufanya wote wafaidi matunda ya elimu. Yaani wasiosoma watafaidi elimu ya waliosoma kupitia miradi ambayo wasomi watakuwa wanaipanga kwa ajili ya jamii yao, miradi isiyo na nia ya ziada zaidi ya kutaka kuikoa jamii husika.
Kwa sasa, kwa nchi kama Tanzania inataka watu wote wahesabiwe wameenda shule japo kufika kwao shule haileti maana kuwa wameelimika ni heri wasingekwenda kabisa kwa kuwa hakuna kitu cha msingi wanachokipata huko. Swala la ubovu wa elimu linafahamika ndio sababu lipo kwenye sera ya elimu ya mwaka 2014 ambayo inatumika hadi hivi sasa. Sera badala ya kuangalia namna yakuboresha elimu inazidi kuhitaji kuongeza udahili wa wanafunzi ili kuongeza idadi ya wahitimu. Ndio maana nimesema inataka watu wote waende shule bila kujali wametoka na nini huko shuleni.
Tunazalisha wasomi ambao badala ya kuhudumia jamii zao wanaziibia jamii zao. Nchi inakuwa ya wahalifu, wanaoumia zaidi ambao ni wananchi wa chini kabisa kwa kuwa hawana wa kumuibia, chuki inapanda juu yao na wanachukiana wao kwa wao kiasi cha kujeruhi kwa makosa madogo. Na hata wakati mwingine wamekuwa wakifanya migomo na maandamano kwa maslahi ya wanasiasa wachache wakiamini kuwa ni njia sahihi ya kufikia maisha bora lakini hata migomo na maandamano pia imekuwa njia sahihi ya wao kufika jela. Vijana wengine hufika mbali zaidi na kisha hufungwa kwa kesi za uhaini.
Lakini kama elimu ikiwa bora, wizi wa wasomi kwa jamii yao hautakuwepo au utapungua kisha wale wasiosoma watafaidi kupitia miradi endelevu ambayo wasomi watakuwa wanaipanga na kuitendea kazi ili kumuokoa mtu asiyetumia muda mwingi shuleni. Kupitia hapo furaha itaongezeka na matukio ya uhalifu yatakuwa yanapungua kisha idadi ya wafungwa itapungua. Hii ndio hoja yangu. Kwa wale ambao bado wana maswali juu ya jinsi ya kupima ubora wa elimu. Naona hii ni njia moja wapo kama taifa katika kupima ubora wa elimu.
Elimu isifundishe ubinafsi, bali imfanye kila mwanafunzi ajue wajibu alio nao kwa jamii yake. Imfanye mwanafunzi kuwa na uwezo wa kupanga mipango ili kuifaidisha jamii yake kwenye long run. Haya yanawezekana ikiwa wanafunzi wataambiwa maana ya maendeleo na misingi ya maendeleo. Maendeleo yakimaanisha ubinafsi huzaa unyonyaji kisha uhalifu, hapa ni wazi kwamba maendeleo ni kitu cha jamii kutoka kwa mmoja.
Tukiangalia hata nchi zenye uchumi wa viwanda hivi sasa, sio kwamba ni raia wote wanchi husika walishiriki katika uletaji wa viwanda, bali wachache walioelimika walileta viwanda kwa ajili ya wengi ili wote wapate kuendelea kwa namna moja au nyingine. Chukulia mtu aliyegundua vifaa vya kilimo kama trekta, yeye atapata hela kwa uuzaji wa trekta lakini mkulima atapata nafuu ya kulima shamba kubwa kwa muda mfupi. Je mwenye trekta anawaibia wananchi kwa kuwauzia trekta?
Lakini kwa hizi nchi zisizoendelea ni kawaida kwa mtu kusema anauza dawa ya mazao kumbe ni maji na hayatibu chochote kwenye mazao. Au mtu anasema anauza mbegu bora kumbe haina chochote ila kwa kuwa tu yeye ametamani kupata hela za watu wa jamii yake bila kuwapa huduma kama mtu aliyeelimika.
Kwa hiyo nnaposema maendeleo ya jamii simaanishi usawa kama ambavyo ipo katika baadhi ya schools of thoughts, bali najua jamii itaendelea kwa miradi ambayo inawanufaisha pande zote, upande wa mgunduzi na upande wa anayepelekewa mradi husika. Msomi asipate hela ya miradi ya kuchimba visima kama visima vyenyewe havitoi maji kama ilivyotokea kwa baadhi ya vijiji hapa nchini, kwa kuwa huo ni wizi kama wizi mwingine.
Lakini hili haliwezi kutokea kama hatutaweka utu kwanza kabla ya hela. Msomi akiweka dhana ya kuwahudumia wananchi kwanza kabla ya hela, wengi watakuwa na furaha badala ya chuki na matukio ya kihalifu yatapungua kwa ngazi zote. Wasomi wa masomo ya humanities tutatarajia watasaidia vijana katika kujitambua ili kujua namna ya kukabiliana na matatizo yao ya kijamii, matukio ya vijana kuchomana visu na bisibisi, matumizi ya madawa ya kulevya nk. Yatapungua.
Naamini hii ni njia sahihi sana ya kuangalia ubora wa elimu, kama wafungwa wataongezeka maana yake elimu ni mbovu zaidi, wasomi ni wezi wanaowafanya wananchi wasiosoma kuzidi kudidimia kiuchumi, wakawa na chuki kiasi cha kufanya uhalifu kama umalaya au ukabaji ili kunusuru maisha yao.
Ubovu wa elimu sio tatizo kwa jamii tu, bali ni tatizo kwa utawala. Watu ambao elimu yao haipo kwa ajili ya jamii zao na taifa lao ila kwa maslahi yao binafsi ni rahisi sana kutumika na watu wanje ili kulidhuru taifa lao kiutawala, kiuchumi au kisiasa. Kama ambavyo inavyoonekana kwa mataifa mengi kushabikia mapinduzi ya kisiasa na kisha wakajikuta sio wao waliohitaji mapinduzi hayo ila mataifa fulani yaliowasaidia kufanya mapinduzi hayo, wao wametumiwa kama chombo bila kujijua..
KAMA WAHALIFU NA WAFUNGWA WATAPUNGUA TUHESABU NI USHINDI KATIKA ELIMU YETU
Muandishi wa makala haya ni mdau wa elimu, msomaji wa vitabu na muandishi wa vitabu.
Co-Author wa kitabu cha MAMBO 100 ya kuzingatiwa na mwanafunzi wa kiafrika karne ya 21
Pia ni host wa blog ya African Positivity