Jemadari Said; kielelezo cha Wachambuzi wa mchongo nchini

Sijawahi kuwa Yanga hili nalisema Kila siku.
Unalisema kwa kujificha tu, ila wewe ni pure Yanga

Sijajua kwanini swala la wewe kujiweka wazi kuwa ni shabiki wa Yanga liwe siri?

Kushabikia Yanga sio aibu come join them, sioni sababu ya kukufanya uishi mafichoni wakati mna kikosi kizuri, mlichukua ubingwa plus unbeaten

NB: Wote tunafahamu kwamba kuwa neutral ni swala ambalo haliwezekani labda kwa unafki
 
😅😅😅😅 Hovyoo kabisa!!, Yaani hata hujatambua kitendo cha Bocco kuuruka mpira nikuhusika moja kwa moja na ufungaji wa gori?, Hujaona kama Bocco kamhadaa gorika?, Hukuona kama Bocco amemkinga gorikipa?.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Hovyoo kabisa!!, Yaani hata hujatambua kitendo cha Bocco kuuruka mpira nikuhusika moja kwa moja na ufungaji wa gori?, Hujaona kama Bocco kamhadaa gorika?, Hukuona kama Bocco amemkinga gorikipa?.
Napenda sana kuheshimu mawazo ya mtu pasipo kutamka maneno yasiyo na maana kama hovyo.

Kuna mechi Messi aliwahi kufunga goli, ilipigwa pasi, foward akaukwepa mpira ili umfikie Messi, hakuonesha interest yoyote ile ya kutaka kuucheza ule mpira na haikuwa offside japo alizidi.

Hakuna tofauti yoyote ya hii ya jana, kama sikosei ni game ambayo Brazil alifungwa na Argentina 3 au 4. Messi alipiga Hat Trick hii game.
 
Kazumari kasha kua kama zuzu sasa hivi amegeuka kuwananga Simba kila kitu anakosoa
Akiwatoa makosa Yanga mnamuita hater na tena hiyo mnaifanya kwa msukumo wa Manara.

Sasa anaisema Simba sijui bado mnamuita hater?

Muache afanye majukumu yake ya kazi, hata Ally Kamwe aliwahi kusema kazi ya uchambuzi haimuhitaji kutengeneza ushkaji na viongozi wa timu maana kufanya hivyo kutakuwa kunamfanya ashindwe kuikosoa timu pale ambapo inakosea
 
Ninarudia tena kwako Scars. Sijaanza Leo kupinga uchambuzi wa Jemadari Said. Mbona Ahmed Ally ni msemaji kabisa wa Simba na sijawahi kumpinga kwa weledi wake? Kanuni yangu kubwa ni kuwapinga wapotoshaji wote. Nimekuwa nikikuelezea kama shabiki unayejitambua lakini unapopuyanga nakwambia wazi hapo uko nje ya mstari.
 
Akichambua sahihi tutamuunga mkono, lakini akitumia platform yake kupotosha Jamii tutampopoa tu.
Mbona tangu jana hajajitokeza kutetea msimamo wake wa goli la Mbeya city kuwa offside?
 
Mimi sikuiti mshabiki wa Yanga kulingana na mtazamo wako kuhusu Jemedari

Na wewe unaelewa sijaanza leo kukuita hivyo na sababu unaijua japo sio lazima ukiri
 
Akichambua sahihi tutamuunga mkono, lakini akitumia platform yake kupotosha Jamii tutampopoa tu.
Mbona tangu jana hajajitokeza kutetea msimamo wake wa goli la Mbeya city kuwa offside?
Ishawahi tokea siku moja ali retweet post ya Shafii dauda inayoonesha makando ya C.O mpya wa Yanga

After few hours, lile swala la C.O kuhusu rekodi mbaya za kiutendaji wa kitaaluma likaja kuwa resolved lakini Jemedari haku update hiyo taarifa mpya

Watu walimuita hater, mchambuzi uchwara na majina mengi yanayoshusha hadhi ya kile anachokifanya.

Lakini Ally Kamwe alienda studio za EFM na akaja kugusia hilo swala wakati huo na Jemedari yupo.

Jemedari alielezea scenario yote vizuri na kutoa sababu za kwanini hakuweka update na mpaka Ally Kamwe anatoka studio alikuwa ameridhika na majibu yake.

Sasa pamoja na hayo yote bado kuna watu ambao hawakumuelewa, sio hawakumuelewa kwasababu hakutoa utetezi wenye mashiko. Nah ni kwasababu washajengewa hiyo dhana kuwa huyo mtu ana chuki na Yanga

Na siku akiwa anaisema negative Simba, utawasikia hao watu wakisema "hana lolote anajifanya kubalansi tu ili aonekane hapendelei upande mmoja"
 
Sisi hatutaki atusifie aendelee tu we need more haters huyu huyu ndio alianziasha uzushi kwamba Nabi hana leseni ya kukaa kwenye bench mechi za CAF
 
Sisi hatutaki atusifie aendelee tu we need more haters huyu huyu ndio alianziasha uzushi kwamba Nabi hana leseni ya kukaa kwenye bench mechi za CAF
Alianzisha uzushi?

Ingekuwa ni uzushi kwanini yule kiongozi wa TFF ali confirm kuwa ni kweli?

Au naye ni mmoja wa haters?
 
Ukiwa kwenye level aliyopo Jemadari au tuseme anayojiweka, hutakiwi kupost taarifa zenye makosa kila wakati ukitarajia kuomba radhi au kurekebisha unapogundulika. Anachokifanya ni makusudi na kudhani wengine hawana uelewa hivyo anaweza kuwadanganya atakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…