Jembe ni Jembe na kundi lako jifunzeni kupokea changamoto

kimpe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
911
Reaction score
862
Ahlan wa Sahlan ndugu zangu naomba niliwasilishe hili kwenu wanajamii na kimshauri huyu brother ninaemuheshimu na kumuona mtu wa kupigiwa mfano kutokana na jitihada zake kimaisha na kusaidia katika jamii.

Huyu bwana alikua muandaaji wa Miss lake zone ambao waliingia kwenye kashfa ya kutaka kutoa gari kuukuu kwa mshindi. Kamati ya Miss Tanzania ikawakalia kooni ukweli kwamba kulikuwa na janja janja kwenye lile.

Sasa jana ndo ikafanyika Miss Tanzania Grand Finale sasa brother huyu ninayemuaminia sana na kundi lake kina Le Mutuz na Wolper wamedhamiria kuchafua shindano hilo kwa kutupa vijembe mbalimbali kuonesha kasoro hata ambazo hazipo mitandaoni.
Mara mshindi kapewa babywalker mara washindi walipangwa kitu ambacho ni kigumu kuamini kama kinazungumzwa na kijana msomi kam yeye kina Le Mutuz Wolper hatushangai.

Ushauri kwake Nimuombe Seba Ndege ajifunze kupokea changamoto na kama kuna jambo lilimkwaza wananjia zao za kulimaliza kuliko Dk Mzima kama yeye kuchamba mitandaoni. Mwanaume hanuni kwa mashavu bwana.
 
Tangu aachane na mke wake kawa mwehu kweli,mara apigane bar,mara azingue watu wakiwa bar,jamaa ana stress sana za maisha!!!
Nami naona sio yule wazamani kumbe kaachana na wife
 
Hata gari la miss Tanzania ni kituko zaidi ya miss lake zone
 
si wakati wa kuwavunja moyo hawa waandaaji waa miss Tanzania. Hakika wamethubutu si rahisi kupata wadhamini ambao wangetoa ndinga (sijui kwanini kila mwaka zawadi kuu imewekwa kuwa gari, nadhani ni ukosefu wa ubunifu) kwa namna ambayo hayo mashindano yalikosa mvuto kwa muda mrefu. Hawa waliokuja sasa angalau wamekuja tofauti na wameonyesha kuwa haya mambo yanaweza kufanyika. Kama kulikuwa na changamoto ni vyema kushauri wa staha si kwa namna ambayo nimeona post ya Wolper kule insta. Hivi Wolper angekuwa ni yeye angeweza kufanya hata 1/8 ya kile kilichofanyika? Kuna baadhi ya watu bado wanaishi kwa sababu sheria haziruhusu kuwatanguliza mahali pema
 
Huyu Basila nae kazingua, kigari gani kile kama cha kuchezea watoto.
 
Basila ka jitahidi warembo walikuwa bomba hata waliohudhuria wameipa heshima yake ni mwaka huu tu mshindi katoka kihalali hamna ulalamishi
 
Basila ka jitahidi warembo walikuwa bomba hata waliohudhuria wameipa heshima yake ni mwaka huu tu mshindi katoka kihalali hamna ulalamishi
naamini akijipanga zaidi na kutofuata yale walioyafanya akina Lundenga, Miss Tanzania itapata hadhi na hata wadhamini pia watapatikana wa maana..... ajipange zaidi ya hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…