Jemedari Said anajua vizuri lugha ya kiingereza, Haji Manara punguza chuki binafsi

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Haji Manara ameishiwa hoja, amesikika akimponda Bin Kazumari kuwa hajui kuongea lugha ya kiingereza, hivyo hawezi kuwa wakala wa mchezaji Farid Mussa, anasema wakala lazima ajue kimombo, akamsifia sana Oscar Oscar kuwa anajua kimombo vizuri na ndio maana anasafiri mara kwa mara nchini Marekani.

Manara amesafiri sana na Simba akiwa nje ya nchi, lini aliwahi kuonekana ama kusikika akiongea lugha hiyo zaidi ya kupiga nao picha, siku moja afanye conference kwa lugha ya kiingereza ili watu wamsikilize akijiuma uma meno, huyo Oscar anayemsifia lini aliwahi kuongea lugha hiyo, kwenda Marekani sio hoja, huyo Kitenge anashinda huko Ulaya lakini hajawahi kusikika akiongea hata siku moja, wachambuzi wanaomwaga ngeli na wanajulikana tumewaona ni Geoffrey Lea, Ibrahim Masoud, Shaffih Dauda, Edgar Kibwana, sio wewe popoma Manara, wala Kitenge wala Oscar.
 
Manara kampiga majungu na kebehi jemedari tena kwa udhalilishaji mkubwa akimsema jemedari kuwa mchafu hapendi kuoga

Lakini mtakumbuka kuwa ameandika hayo muda mfupi uliopita baada ya kulalamika kuhusu tabia ya wabongo kumsema kupitia ulemavu wake.

Hapo ndio nakumbuka maneno ya jemedari aliyojibu malalamiko ya manara

Kuwa ni kweli tabia hiyo sio nzuri na haifai kuigwa ila manara una leta double standards maana hata wewe umekuwa ukiwaponda wengine kwa mapungufu yao.

Ulishawahi kumuita mwakalebela ana kilo 800, ile ni weakness yake naye hapendi kama ambavyo wewe usivyopenda kuona mtu ana kashifu albinism yako.
 
Kiingereza sio kipimo cha Akili.

Mo Dewji hajui kiingereza cha kuongea vizuri ila anapesa nyingi kuliko Senzo Mbatha CEO wa YANGA SC.
 
Wewe inakuuma nini ?ugomvi wa haji manara na kazumari kipi kinakukeleketa?na huyo kazumari uwa usikii vijembe anavyovirusha kwa manara?achana na manara una maisha yako fuata utaachwa na dunia oohooo
 
Hapa tupo pamoja mtani Manara anazingua sana
 
Hajui kiingereza na wala hajui hata kuvaa wakati eti ni wakala wa wachezaji
 
Jemedari yupo pale kuichafua Yanga,na hakuna namna huyo Kazumari inabidi achafuliwe yeye mwenyewe.........na kazi hiyo anaachiwa Haji Manara

Hakuna cha kumuonea huruma mtu
Manara is here to stay
 
Huyu Haji aliopokuwa Simba alikuwa anamtuhumu Oscar na Kitenge kuwa wanaenda sana marekani kufuata mabwana zao, leo anasema Oscar anaenda marekani Kwa sababu anajua kimombo. Huyu Haji akili zake zinamtosha kweli au ugoro umeshaanza kumuathiri?
 
Kingereza kwa watanzania wengi ni mtihani sana kuna viongozi wengi wa nchi na raia wa kawaida hawajui na kwanini hatujui hatukitumii mara kwa mara kitu kama hukitumii huwezi kukielewa vzr
Hivyo hii ni kawaida sana kwa mtu aliyekaa nchi kutoshangaa watu kitojua kingereza huyo Hajii mwenyewe anajua wazi hata yeye hajui kuongea kingereza hivyo anatafuta domo lake kila siku lionekane anaongea hata kama hamna logic yeye anaongea
 
Kingereza siyo ishu kubwa,hata Rais wetu wa awamu ya tano kingereza kilikuwa shida lakini alikuwa anapiga kazi kinoma ukiachilia mbali mapungufu yake mengine
 
Kuna viwango vya kujua na kuongea lugha, alichosema Haji shida aliyonayo Kazumari ni kutengeneza sentensi Moja iliyo nyooka ya Kingereza. Wakati uo uo yeye ni meneja wa baadhi ya wachezaji kinachohitajika ni Jemedari kusoma na kuielewa iyo lugha ki ufasaha ita msaidia katika shughuli zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…