DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,983
- 11,857
Maoni yangu kuhusiana na muda/ dakika zinazoongezwa baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika (additional or added minutes), maoni yamejikita kwenye ukweli na uhalisia wa jambo lenyewe kwa wale ambao hawana uelewa kuhusiana na huu muda/dakika za nyongeza.
MPIRA NI MCHEZO WA MAKOSA
Kagere kukosa penati na kudhani kwamba amefanya makusudi ni kumkosea heshima mchezaji. Ukweli kwamba Kagere amewahi kuwa mchezaji wa Simba haina maana yoyote au uhusiano wa Kagere kukosa penati ya jana ambayo iliipa Simba ushindi wa 3-2 baada ya sare ya 1-1 kwa dakika 90.
Ni bahati mbaya (coincidence) kwamba imetokea hivyo ila kwa utamaduni wa mpira wetu kinachoendelea ni kitu cha kawaida na tumekiruhusu, jaribu kufikiria kwamba kama ingekuwa ni mechi ya Simba na Yanga. Simba walibeba ubingwa wa Afrika Mashariki mwaka 1992 pale pale Amaan kwa matuta wakiwafunga Yanga, penati ya mwisho ya Yanga ilipigwa na David Mwakalebela na Mwameja akadaka, mpaka leo watu hawajamsamehe Mwakalebela.
Chibe Hamidu Chibindu akiwa Yanga naye aliwahi kukosa penati katika penati tano tano Mwameja tena akadaka, Simba wakaja kuibuka Mabingwa wa FA Cup kama sijakosea, mpaka leo wapo ambao hawajamsamehe Chibe Chibindu.
Naamini Kagere hakuwa na nia ya kukosa ili kuwapa nafasi Simba, ni sehemu ya makosa kama yale ya Gadiel Michael ambaye alicheza Simba na yale ya Kennedy Juma ambaye aliwahi kucheza Singida, hawakufanya hivyo kulipa fadhila kokote ni makosa tu, soka ni mchezo wa makosa.
NB: Walipofungwa Yanga 3-1 na APR, waliolalamika zaidi ni Simba, jana wamefungwa Singida wanaolalamika zaidi ni Yanga, sijui uhusiano uliopo.
BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)