Elections 2010 jenerali: Nukuu ya kunukulika!!!

minda

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2009
Posts
1,068
Reaction score
67
mwanazuoni jenerali anatuambia:

"Tunachagua kama vipofu, kisha tunalalama kama vichaa. Sasa tuamue: ama tuchague viongozi wetu kwa makini, au tukae kimya wakati wakitunyanyasa. Wachagua hovyo wasiwe wasema hovyo wakitendewa hovyo."


:dance: wakuu hii imekaaje?


Source: Raia Mwema
 
hii niliipenda sana

ni kweli ukichagua hovyo usiseme hovyo!
 

Na asiyeenda kuchagua kiongozi ameshiriki kuchagua viongozi wabovu naye asilalamike.
 
Walalamikaji wengi huwa hawashiriki kwenye kupiga kura kisha kujisifia wao walijua mambo yataenda vibaya ndiyo maana hawakuchagua mtu.
 
Mi nadhani Jenerali anawaonea tu watu wengi tu wanaokwenda kuchagua kiusahihi -- yaani wale wanaotaka mabadiliko. Sasa kama CCM wanafanya kila hila kama vile kuiba kura hao pia utawaita walichagua hovyo? Nao pia wakae kimya. It's not fair to say so, Jenerali.
 
the best of the best... inatakiwa wapinzani waibebe kama ilivyo na kuweka kwenye moto yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…