Jenerali Ulimwengu alikuwa na bifu gani na Hayati Magufuli?

Jenerali Ulimwengu alikuwa na bifu gani na Hayati Magufuli?

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Leo nimejikuta nawaza!

Nini hasa ambacho kipo nyuma ya pazia kati ya Hayati Magufuli na Jenerali Ulimwengu?

Msingi wa swali langu unatokana na maneno ya Jenerali Ulimwengu kwa Hayati Magufuli! Sijawahi kumsikia Mzee Ulimwengu akimsema Magufuli kwa mazuri, na hili limeingia mpaka kwenye gazeti lake la RAIA MWEMA.

Mzee Ulimwengu namfananisha na Mzee kule Club House nahisi anaitwa "Abiud" yeye ata ukimuuliza nitajie zuri moja tu la Magufuli ye atakujibu hajawahi kuona hata punje ya zuri lake always kila alilofanya Magufuli lilikuwa baya.

Angalia kichwa cha habari cha gazeti la leo la Raia Mwema.

20220824_082255.jpg
 
Kila mtu ana perception yake anapomzungumzia mwingine, ukiona Ulimwengu anakukera anavyomsema Magufuli vibaya kila siku, wapo jamaa huku hunsifia Magufuli kila siku, wasome hao.
Hao wanaosifia wapo wazi kabisa kwamba ni mashabiki wa Magufuli au walikuwa wakimsifia kwa manufaa yao binafsi, ila watu aina ya Ulimwengu inaleta shida kujua anachofanya ni kukosoa au ni chuki aliyonayo kwa Magufuli.
 
Huyo kila utawala huwa anakuwa na bifu nao. Hata huyu mama akimaliza asipompa hata uenyekiti wa bodi fulani akimaliza muda wake utaona anavyomuandama.

JK alipomaliza alianza kumuandamana, ndipo pale ilipotoka kauli kuwa viongozi waliostaafu waachwe wapumzike.
 
Dini
Hujiulizi kwanini huwashambulia nyerere,mkapa na magufuli tu?
Ni nadra Sana kumkuta Ulimwengu anamsema vibaya Nyerere ila Mkapa walikuwa na bifu kwa kiasi furani linahusiana na ukosoji wa mara kwa mara kutoka Kwa ulimwengu.
 
Ni nadra Sana kumkuta Ulimwengu anamsema vibaya Nyerere ila Mkapa walikuwa na bifu kwa kiasi furani linahusiana na ukosoji wa mara kwa mara kutoka Kwa ulimwengu.
Ila Ulimwengu wa miaka ya tisini na 2000 alikuwa anaandika vizuri sana.
Nimemsoma sana wakati ule, makala zake zilikuwa zinafikirisha sana. Ila Ulimwengu wa sasa hasa anapoongea unaona kabisa ana kaujeuri ka kisomi.

Alikuwa swahiba sana wa Mkapa, tena alikuwa kwenye timu yake ya kampeni mwaka 1995.
 
Back
Top Bottom