Jenerali Ulimwengu katuandikia kitabu- Rai ya Jenerali

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
1628673684674.jpeg

Judge Joseph Sinde Warioba at the launch of the RAI YA JENERALI book on 06. 08. 2021.
 
Hichi Kitabu Kitakuwa na Kile Kinachostahili Kwa Jamii ya Watanzania Kwa Maana Mwamba huyu Habahatishiga pale anapoamua kuitumia Kalamu yake basi Anaitendea haki Elimu yake. Hao wengine sijui Maprofessor Hakunaga Kitu na Ndio maana Wanajidharau hata wenyewe "Prof utatolewaje Jalalani" only in Tanzania.
 
Umekipata na kukisoma mkuu?
 
Makala zake nyingi nilizisoma wakati ule akiwa mmoja wa wamiliki wa gazeti la Rai chini ya Habari Corporation. Wakati ule timu yao ya waandishi nguli ikiwa imetimia haswaa

Pamoja naye Jenerali Ulimwengu kulikua na Salva Rweyemamu(aliyekuja kua mkurugenzi wa mawasiliano ikulu wakati wa JK), Johnson Mbwambo, Dr Gideon Shoo, Francis Chirwa(hasa kwenye michezo) na huku Joseph Mihangwa akiwa anachipukia kiuandishi

Makala za "Rai ya Jenerali" ziliandikwa katika uandishi uliotumia akili nyingi sana. Jenerali alichambua matatizo ya mfumo wa kisiasa, kijamii na kiuchumi wa nchi yake huku akikikosoa chama chake cha mapinduzi(sina hakika angali mwanachama wake}, akimkosoa Rais wa nchi tena wakati ule akiwa Rafiki yake Ben Mkapa kwa uwazi kabisa

Jambo hilo lilikuja kumletea shida hadi akanyang'anywa uraia wa Tanzania na huku mwenyewe akisema hawakumwambia yeye ni raia wa nchi gani. Ikumbukwe kua Jenerali Ulimwengu ndie alikua kampeni meneja wa Ben Mkapa mwaka 1995. Sijui walikuja kutofautiana kitu gani(japo nahisi ni namna ya nchi ilivyokua inaongozwa). Nadhani hasira za Ben Mkapa ni kuona Rafiki yake mwenye kujua siri zake za ndani kabisa anaunanga na kuuchanachana utawala wake kupitia kalamu yake

Jenerali Twaha Ulimwengu alikua ni miongoni mwa wabunge 55 walikua wakijulikana kama G55 ambao miaka ya mwanzo ya 1990s(uhakika ni 1993/4) walioanzisha vuguvugu la kudai muundo wa muungano wa serikali tatu. Kama sio Mwalimu Nyerere kulipinga jambo hilo kwa nguvu zake zote kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kubomoa hoja za washindani wake jambo hilo lingefanikiwa

Waziri Mkuu wa wakati ule John Malecela alilazimika kujiuzu kutokana na shinikizo la Mwl. Nyerere ambaye alimuona kama ameshindwa kuilinda katiba hadi kufikia kutaka kukubaliana na hoja ya kundi hilo
 
Jamaa alieleza chanzo Cha ugomvi wao ilikua kuna waziri wa mkapa alikua mwizi wao wakamuibua cheki interview yake alifanya tv E
 
Asante kunikumbusha mkuu. Nimeshamkumbuka hata huyo Waziri mwenyewe. Tena aliwahi kuhudumu kama DG wa TISS Enzi za Mwalimu Nyerere. Issue yenyewe ilikua inamuhusu mkewe na malipo tata ya matibabu nje ya nchi
 
Kitabu kinapatikana wapi kwa maana ya duka ndugu yangu
 
Asante kunikumbusha mkuu. Nimeshamkumbuka hata huyo Waziri mwenyewe. Tena aliwahi kuhudumu kama DG wa TISS Enzi za Mwalimu Nyerere. Issue yenyewe ilikua inamuhusu mkewe na malipo tata ya matibabu nje ya nchi
Dah nilimsikiliza mzee yuko humble sana kwanza ni mwanasiasa na mwandishi aliyebobea ni mwanaccm asiyekua mnafiki nilimsikiliza kuna sehemu akawa anatoa hoja ya uhuru wa kujieleza akasema hauwezi kuruhusu vyama vingi ukazuia uhuru wa kujieleza pia kwenye suala la mgombea binafsi akasema kuna maeneo watu wanawanyima haki ya kuwatumikia watu eti kisa Hana chama
 
Humjui vizuri
 
Tuambie unavyomjua wewe
Ugomvi wake na Mkapa -Jenerali aliagiza apewe ubalozi siyo ubalozi tu bali ubalozi wa Ufaransa kama malipo ya mchango wake kwenye kampeni ya Mkapa 1995. Mkapa akamtolea nje.
2. Alimtishia Mkapa kwamba anasiri ya waziri wake na kwamba asimpomfukuza uwaziri ataendelea kumuandika. Siri aliyokuwa nayo alipewa na Membe ambaye alikuwa na ogomvi na huyo waziri wa Mkapa.
 
Waziri mstaafu huyu

Simuelewagi au kweli sigara anavutaga kama wanavosemaga

Uvaaji wake marazote nachekaga
 
Ugomvi wake na Mkapa -Jenerali aliagiza apewe ubalozi siyo ubalozi tu bali ubalozi wa Ufaransa kama mchango wake kwenye kampeni ya Mkapa 1995
Nadhani Kama nakuelewa hayo mambo yapo lakini hiyo ndio mfumo wa siasa hasa nchi za kiafrika hususani Tanzania na CCM kwa ukubwa maana hivi vyeo vingi vya uteuzi kazi yake ndio
 
Unamtisha halafu mtu mwenye Mkapa tena siyo Mkapa tu Rais Mkapa= kwa ujumla Jenerali Ulimwengu ni mtu CARELESS sijui neno zuri na fupi kwa kiswahili
 
Back
Top Bottom