Beira Boy
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 19,976
- 32,195
Amani iwe nanyi wapendwa katika bwana,
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu,
Lilikuwa ni jeneza la mama mmoja ambaye alikuwa ni mama ntilie lakini alikuwa tajiri sana akiwa anamiliki majumba makubwa ya kifahari na magari ya maana kwa kifupi alikuwa don lakini kazi yake ni umama ntilie kitu ambacho watu walikuwa wakijiuliza sana kuwa katoa wapi hela zote hizi za kufanya vitu vikubwa wakati ni mama ntilie tu.
Siku ya kifo chake aliuawa kwa kuchapwa mapanga na watu waliomtangizia usiku akiwa anarejea kwake, watu hawo walikuwa wamebebana kwenye boda boda, walimpiga mapanga hadi kifo kumkuta, akiwa anapelekwa hospitali baada ya damu kuvuja nyingi sana.
Sasa ndugu walikaa na kupanga siku ya mazishi na ilibidi akaombewe kanisani maana kanisa lile huwa lina kautaratibu ka marehemu kulala kanisani kabla ya siku moja kuzikwa.
Safari ilianza ya kumtoa mochwari na kumpeleka kanisa la ST JOHN parokia ya Nyampande huko Sengerema Mwanza, walifika tu vizuri na kumshusha kwennye gari vizuri tu.
Sasa wakati wanamuingiza kanisani jeneza liliongezeka uzito na kulishusha upesi sana, wanaume na nguvu zao zote walijaribu tena kulibeba jeneza lile ili wamwingize kanisani lakini wapi, walijitutumua kwa kuliburuza lakini walipofika mlangoni jeneza liliongezeka upana na kufunga mlango lisiweze kuingia.
Hili tukio liliacha mdomo wazi watu wengi sana nikiwemo mimi maana mimi nilikuwepo pale kanisani nikiwa mtumikiaji wa zamu kwa siku hiyo.
Ilibidi baba paroko awambie waliache jeneza hilo hapo hapo nje wafunge turubai, walifunga turubai kwa nje wakafanya maombezi.
Mimi hadi leo huwa sielewi kwanini jeneza lile liligoma kuingia kanisani? Je mama yule alikuwa na zambi nyingi sana au ni kitu gani?
Nawasilisha
LONDON BABY