Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JENGO LA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA
Lango kuu la kuingia jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) lililojengwa katika miaka ya mwanzoni miaka ya 1930 leo lina maandishi: "OFISI YA RAIS (TAMISEMI) HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM SHULE YA MSINGI LUMUMBA..."
Nini historia ya jengo hili na taasisi yake?
Historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika inaanza na historia ya African Association (AA).
Waasisi wa African Association na wanachama wengi wa African Association walikuwa Waislam na halikadhalika uongozi wake.
Kleist Sykes kaeleza katika mswada wa kitabu chake kwa nini ilikuwa hivi.
Kwa sababu hii ikawa mambo mengi ambayo Waislam waliona hawatendewi haki na Waingereza yakawa yanapitishwa kupitia AA.
Hii ikaonekana si sawa na ndiyo wakaamua waunde Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 pembeni ya AA ili ishugulikie matatizo ya Waislam.
Viongozi wa juu wa Al Jamiatul Islamiyya fi walikuwa Kleist Sykes, Mzee bin Sudi na Ali Jumbe Kiro.
Huyu Ali Jumbe Kiro alikuwa rafiki mkubwa wa babu yangu Salum Abdallah.
Viongozi hawa wakaamua kujenga shule kwa ajili ya watoto wa Kiislam kusomesha Qur'an hapo shuleni.
Aga Khan alipotembelea Tanganyika mwaka wa 1936 alitembelea shule ambayo ilikuwa inajengwa na yeye akaamua kuchukua jukumu la kuijenga na kuikamilisha.
Hii ndiyo shule aliyosoma baba yangu pamoja na watoto wengi wa Dar es Salaaam waliozaliwa miaka ile ya 1920.
Hafla ya kumuaga Julius Nyerere safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika kwenye jengo hili.
Utajiuliza iweje shughuli ya TANU ifanyike Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Ali Mwinyi Tambwe alikuwapo katika mazungumzo yaliyofanyika mwaka wa 1953 nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio kati ya Mwapachu na Abdul Sykes kuhusu kumtia Nyerere kwenye nafasi ya juu kabisa katika uongozi wa TAA.
Ali Mwinyi ndiye alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Lakini pia Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Iddi Faiz Mafungo ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere UNO na alikuwa pia Mweka Hazina wa TANU.
Serikali ilipoivunja East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuunda BAKWATA jengo hili likawa chini ya BAKWATA na mwishowe ndiyo hivi liko chini ya TAMISEMI.
Katika uhai wake Ally Sykes alijitahidi sana jengo hili lirejeshwe kwa wenyewe Waislam lakini hakufanikiwa hadi anaingia kaburini.
Tunao ujasiri wa kuhifadhi historia hii na nyingine kama hii tukaweka vibao (plaque)kueleza yaliyofanyika katika majengo hayo?
Je, tunao ujasiri wa kuisomesha historia hii katika shule zetu?