A
Mzabuni angekuwa ameshalipwa kila anachostahili kwa mujibu wa mkataba na bado asiendeleze ujenzi wangeshamchukulia hatua stahiki.Ajabu ni kwamba unaweza kukuta pesa alishalipwa mzabuni
Waliambiwa WajipimieMimi ni mwananchi wa Singida, kero yangu ni jengo la ghorofa sita kwaajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, lilianza kujengwa tangu nipo Sekondari Miaka ya 2010's lakini mpaka leo ujenzi wake haujakamilika.
Kuna jengo la ghorofa 6 linaitwa Covid 19 sijui, yaani kuna majengo mengine ya hospitali nyingine za mikoa mingine yamejengwa na kukamilika ila hilo ninalolieleza hapa lipo ghorofa ya kwanza, halijaisha na linasuasua miaka na miaka!
View attachment 3572454
Waziri Mkuu alipotembelea Jumamosi, Agosti 06, 2022 kukagua ujenzi wa hospitali hiyo ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 19.
View attachment 3572456
Mawaziri, Katibu Wakuu wa Wizara za Afya washatembelea pale mara kibao lakini sioni maendeleo yeyote, mara nasikia watu walikula pesa sijui ngazi ya Wizara au Hospitali? Sielewi mimi.
Hospitali kama ka-kijiji, hakavutii, viwodi vichache vimeungana ungana hovyohovyo!!
Siasa nyingi, majibu zero!!
Nauliza hilo jengo litakamilika lini? Na kama kuna jitihada ya kulimalizia mapema ili lihudumie wananchi.
Miaka zaidi ya 10, hospitali haijaisha? Inatia hasira! Halafu ndo na waziri mkuu anatokea hukuhuku🙄🙄🙄🙄 Ngachoka mimi.
Orodha ya hao viongozi wanaokuja hapo kila wakati na maendeleo ya ujenzi ni indirect proportional.
Sasa kama alilipwa kisha akawakatia 10% wakubwa unadhani nani atakuwa na ujasiri huoMzabuni angekuwa ameshalipwa kila anachostahili kwa mujibu wa mkataba na bado asiendeleze ujenzi wangeshamchukulia hatua stahiki.
Naamini shida ni kwa mamlaka wenye mradi, yaani serikali.
Kama mzabuni huyo aligawana na wachukua hatua ni na nani atakayechukua hatua hizo?Mzabuni angekuwa ameshalipwa kila anachostahili kwa mujibu wa mkataba na bado asiendeleze ujenzi wangeshamchukulia hatua stahiki.
Naamini shida ni kwa mamlaka wenye mradi, yaani serikali.