DOKEZO Jengo la RITA Tower lina ghorofa 26, linatumia lift 1 tena ya kizamani, ukiingia unatoka umeloa jasho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
​
Jengo la RITA Tower lililoko Posta Dar es Salaam, naona wameamua kulisahau mpaka siku maafa yatokee ili waunde tume.

Jengo lile lina ghorofa 26, mnaweza kuelewa limebeba watu wengi kiasi gani lakini cha kusikitisha ni kwa lift za jengo lile ni nne (zilianza kufa kuharibika moja baada ya nyingine na mpaka sasa lift inayofanya kazi ni moja tu.

Imegeuka kero maana Watu ni wanafanya kuigombania hasa wakati wa kupanda, unajikuta unamaliza nusu saa na zaidi ukisubiria lift, maana haiwezi ku-accomodate watu wote.

Tunaomba uongozi wa jengo hilo ufanyie kazi matengenezo ya lift zote zifanye kazi, inakuwaje ghorofa 26 kuwa na lift moja tu! Siyo sahihi na lift zenyewe ni zile za kizamani mkirundikana humo mkishuka mnachuruzika jasho mwili mzima.

Pia soma ~ Lift moja kati ya zilizokuwa hazitumiki katika jengo la RITA Posta imeanza kutoa huduma

Bahati mbaya ni kwamba viongozi na maboss wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wakifika, lift hiyo pia huzuiwa na wanapandishwa wenyewe kwanza, tunauliza na wao hawalioni au mpaka siku maafa yatokee ndio watazitengeneza? na kuunda tume kama tulivyozoea?


​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…