Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Salim Uhuru, mkuu wa timu ya uokoaji amesema kuwa, miili ya watu sita imetolewa kwenye kifusi na kupelekwa kwenye kitengo cha kuhifadhia maiti mjini Kampala kwa ajili ya kutambuliwa.
Kwa mujibu wa Bw. Uhuru, jengo hilo liliporomoka milango ya saa nane mchana jana na taarifa za awali zilisema watu watatu wamepoteza maisha na wengine wengi wamefukiwa na vifusi.
Amesema juhudi za kutafuta wahaga zaidi zinaendelea huku waokoaji wakipata matumaini ya kupata watu wakiwa hai hasa baada ya watu saba kuokolewa wakiwemo watoto wadogo wawili.
Watu walioshuhudia wamesema, kuna uwezekano kusiwe na watu wengi walioangukiwa na jengo hilo hasa kutokana na ishara za kuporomoka kwake kuonekana mapema na kutoa fursa kwa baadhi ya wafanyakazi kukimbia.
Kwa upande wake, Shirika la Msalaba Mwekundu limetoa taarifa na kusema kuwa, limetuma timu yake ya uokoaji yakiwemo magari ya wagonjwa kwa ajili ya kusaidia zoezi la uokoaji.
Chanzo: Jengo laporomoka Uganda na kuua na kujeruhi watu wengi