Jana ITV walimwonyesha mdada moja anayetegemewa na wadogo zake, babake amestaafu, anayeishi mbagala, wanasema vyuma vimeingia kwenye mwili wake, ni mtu wa kulala tu, walionyesha plastic ya mkojo anajisaidia palepale kila kitu, na ni mtu wa kitandani. anasema, pale muhimbili wamesema hawana uwezo tena wa kumtibu, labda nje, sasa alikuwa anaomba msaada watz wamsaidia kumchangia ili aende nje. SWALI: JWTZ etc au serikali kwa ujumla, imewafanyia nini hawa watu? iko wapi hadi watu hawa wanaomba msaada kwa wananchi wakati wao waliomsababishia matatizo wamemtelekeza?