Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameiomba Hospitali ya Queens iliyopo jiji la London nchini Uingereza kutoa ushirikiano kwa Tanzania ili msukumo wa kuimarisha huduma za Afya uzidi kuimarika.
Waziri Mhagama amewasilisha ombi hilo Desemba 11, 2024 wakati akihutubia mkutano wa uongozi wa hospitali hiyo wenye lengo la kusaidia kwenye nyanja mbalimbali na kuimarisha huduma za afya nchini ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba, dawa pamoja na kubadilisha uzoefu wa wataalam wa afya.