Jenista Mhagama: Tutatimiza agizo la Rais la kupandisha mishahara kwa wakati

Kumbe mishahara hupanda kwa agizo la Rais na si takwa la kisheria - kumbe eeee

kidumu chama cha mapinduzi...
 
Mbona tulishakubaliana tusitangaze ,maana wafanyabiashara watapandisha Bei kwenye bidhaa,au mmesahahau?
 
1. Sheria gani mtazingatia kupandisha mshahara?
2. Mishahara haijapanda tangu 2015 kinyume na sheria inavyotaka kila mwaka mshahara unaongezeka kwa asilimia iliyoinishwa
3. Viwango vya mishahara, posho na marupurupu yaliyoainishwa kwenye sheria za kazi [ELRA 2007 with subsequent miscellaneous amendments] havikuwa vinarekebishwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria kufanyika kila baada ya miaka mitatu, je serikali iko tayari kuongeza pamoja na mapunjo ya miaka saba iliyopita?
4. Kiwango cha kodi ya PAYE (Pay As You Earn) kwa mishahara inayoangukia kwenye asilimia 18%-30% na yenyewe ishushwe na kuwa na uwiano wa 12%-25% kutoa unafuu kwa wote sio kima cha chini pekee ambacho kwa sasa nio asilimia 8%
 
Ni vyema kuongeza kwanza kabla ya kushughulikia hayo mengine. Kuliko kuendelea kusubiri wakati watumishi wameumia tangu mwaka 2015.
 
Lile jambo letu, waseme hata jambo lina asilimia ngapi bas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…