The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
IDADI ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa ukimwi nchini vimepungua kutoka 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka jana.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizindua Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids).
Alisema hali hiyo imetokana na afua mbalimbali za afya zinazofanyika nchini katika kupambana na ugonjwa huo.
"Takwimu hizi zinaonesha ama matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARV) yameongezeka, ama watu wanaopima na kufahamu hali zao za kiafya imeongezeka," alisema.
Alisema pia kiwango cha maambuzi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU) kimepungua kutoka asilimia saba mwaka 2003/2004 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/2017.
Kuhusu maambukizi mapya kwa watu wazima, Jenister alisema idadi ya watu wanaopata maambukizi mapya imepungua kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka jana.
Aidha, alisema kiwango cha maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia saba mwaka jana.
Hata hivyo, Waziri huyo alisema kuna haja ya kutiliwa mkazo maeneo mbalimbali ya afua za kupambana na ugonjwa huo, ikiwamo kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Kasper Muya aliwataka wajumbe wa Kamisheni hiyo kuangalia watu wenye ulemavu wanafikiwaje na huduma za VVU na ukimwi.
Alisema kumekuwapo na changamoto ya watu wenye ulemavu kufikia huduma zinazotolewa na kusisitiza huduma ziwe rafiki.
Muya pia aliitaka Kamisheni hiyo kuja na mikakati itakayowezesha mapambano dhidi ya ukimwi yanakuwa endelevu kwa kutegemea fedha za ndani.
Chanzo: HabariLeo