Jerry Muro aivua nguo Yanga, adai kuna wanafiki

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema kuwa ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri.

Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake.

“Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka”. Amesema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.

Muro ameongeza kwa kusema kuwa “Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga”

“Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake yamemshinda”

Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mpende na jirani, kaka kama MTU kashindwa kuendesha familia yake kamwe hawezi kuendesha Yanga”. Muro ameyasema hayo kupitia chombo cha habari cha UFM radio

Chanzo: Bongo5
 
Anasema leo baada ya kuteuliwa msemaji mwingine?
Angeinekana wa maana kama angesema enzi hizo!!

Maneno ya mkosaji
 
Reactions: PNC
Kunyamaza kunajenga heshima sana. Tatizo sio kila mtu anaweza kunyamaza.
 
Kuna watu kweli wanapenda usemaji wa Yanga pamoja na kung'atuliwa bado tu anajitahidi kuisemea Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…