Jerry Muro amtusi tena Haji Manara

Mnamuombea sana Jerry Muro aachishwe kazi na Yanga SC. Kama kufukuzwa angelikuwa kafukuzwa tangu kitambo.

Tunajua umuhimu wake haswa kwenye Propaganda za Upinzani wa simba na Yanga.
 
Kuongea maneno kama hayo tena kwenye media, inayosikilizwa na watu wa rika mbalimbali ni kukosa weledi wa kazi anayoifanya...hana ethics za kuwa msemaji! Hata kama ni watani yapo ya kusema lakini siyo hayo. Anafaa kuchukuliwa hatua za kinidhamu!
 
Mbona kikwete alisema maneno machafu sijui kachomeka mara hakuna alichochomeka wala hachomoi na bado mlikaa kimya sana mkaona ni utani haya sasa ila yanga si wana undugu na ccm may be wanafundishana hiyo mipasho
 
Hayo mashindano ya kimataifa wameanza kushiriki mwaka huu? Mbona miaka ya nyuma hakukuwa na malalamiko ya ratiba kama kipindi hiki? TFF ya malinzi imeshindwa kuficha hisia zao, na ni JIPU!
 
Acha ushabiki hapa!! Simba wanataka Ubingwa wa Mezani, kitu ambacho hakipo!!

Hakuna anae kurupuka kutukana kama ww hujamtukana.
We jamaa inaonyesha ni shabiki maandazi, kati ya timu inayomaliza mechi zake mapema na inayochelewa kumaliza ipi ina nafasi ya kuchukua ubingwa wa kupanga matokeo?! Alafu na yeye Muro ana kipele kinamuwasha, kwani Azam fc hawana msemaji wao mpaka awasemee?!
 
Uyu muro haonyeshi uexpart wake ktk tasnia ya habar mm nadhan watu kama hawa ndo wanakakwamisha mpira wetu sidhan kama ana sifa za kua msemaji was klab kama yanga
 
Labda mimi nijikite kisheria zaidi kama nitakua nimepitia vizuri hiyo nukuu yako na kama utakua umenukuu vizuri yale yaliyotamkwa na Muro.

Sijaona katika nukuu hii jina la huyo anayetajwa kuzunguka kutwa nzima akizumgumzia mambo ya Yanga na Azam kwamba limetajwa kua ni Haji Manara, nukuu yako ni hii "Mtu mzima na akili zako tena Mtoto wa Kiume unaacha kufanya mambo yako kutwa UNAWASHWA WASHWA na kuzunguka huku na kule kuzizungumzia Yanga na Azam kama siyo anataka KUKUNWA huyu anataka nini? ".

Mtu unaweza kuyasikia maneno na kuyaona kihisia yanamgusa mtu fulani na ukaona uko sahihi kabisa, lakini hakuna namna utathibitisha kwamba alikua anamlenga huyo unayemdhani. Unless umeacha baadhi ya maneno katika nukuu yako, lakini kwa hapo sioni namna tutasema Muro anamzungumzia Manara. Nayaeleza haya nikiwa mtu huru nisiyefungamana na upande wowote, kati ya Simba, Yanga au Azam.
 
jery inabidi aache uswahili awe anatumia maneno yenye staha na faida kwa klabu....

hayo maneno hayana mantiki yapo kihuni sn.
 
Kwenye quotation "Mtu mzima ..... " mbona sijaona sehemu yeyote akimtaja mtu jina? Umejuaje anamwongelea Haji Manara?
 
Kwa kuanza na uongo kumekufanya usiaminike.
 

Tunashukuru kwa kuwapotezea muda Walimu wako wa SHERIA huko Chuo Kikuu kwani umeonyesha udhaifu mkubwa sana wa kiakili na umeivamia hiyo fani. Siku hizi kila mtu ni mwanasheria.
 
Kama huna mahaba na soka wala hufuatilii mpira, umejuaje EFM ina mahaba 90% na machampioni Yanga? Mikia mmeanza kuikimbia mbumbumbu fc?
 
Hao wote ni "waswahili" kinachotokea ni kuzidiana extent ya kuongea "shombo"!
SHOMBO!!!!!!?? Au Matusi!!? Hivi Ukiambiwa Kuwa UNAWASHWA!! Unatafuta Mtu AKUKUNE!!! Ni Shombo Hizo Au Matusi!!!?
 







Nafikiri wanaowashwa na ambao wanahitaji kukunwa ni hao hapo juu.Tangu TFF imfungie Juma Nyosso tabia hii imekuwa sugu kwa Yanga.Naomba TFF iliangalie hili kwa jicho la huruma na imfungulie Nyosso ili aje atulize mizuka ya wachezaji hawa.
 
Mkuu Mpema hakika picha yako imenichekesha, Unajua kuna maneno yasemayo "mtu hunena yaujazayo moyo wake"Nahisi hizo kauli zinalingana na tabia hizo kwenye picha.
 
Manara aache kiherehere. pengine kwao na akina Muro wanazijua dalili za mtu anayetaka kukunwa.
kwetu mtu anayetaka kukunwa hukunyang'anya kitu (kama kofia,kilemba nk) kisha hukimbilia kichakani.
siwezi kuhumu hapo.
 
Niliwahi kuleta mada hapa kuhusu Jerry Muro nikasema asaidiwe ana tatizo la kisaikolojia baadhi ya wadau wakaona kama mzaha. Moja kati ya heshima kubwa ya binadamu ni kuwa na break mdomoni. Michezo inahusisha watu wa rika mbalimbali na heshima kubwa katika jamii. Maneno ya kihunikihuni na kuropokaropoka hayapaswi kutolewa na mtu mwenye hadhi ya kuwa msemaji a.k.a 'mdomo' wa klabu kuwa kama Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…