Jerry Muro: From ITV to TBC1


Ahsante kwa maelezo mareeeeeeeeefuuuuu. Sasa jibu swali.
 
Ni kweli jamaa haonekani tena ITV, nilimpenda bure na kazi yake very open especially na kile kipinidi cha RIPOTI .........

Naomba ufafanuzi wa hiyo red kabla sijatafuta kamba.
 
Jeryy yuko mjini nasikia anahamia TBC baada ya kutoelewa na ITV maswala furani!!.
 
Bado Yupo Yupo TU - ITV hamna HRM (Afisa Uajiri) kwahiyo hawezi kufukuzwa kwa kuwa alikuwa hajaajiriwa. The thing is, yale makubaliano maalumu (aka Contract)na JM yamekamilika muda wake na yeye sasa ana haki ya kuanza mbele kwa maana possibility ya renewal ni kama hakuna.

Anywayz, siku njema
 

yaani kituo kikubwa kama itv hakina hr section
haaa sehemu zingine basi ukifanya kazi naona hakuna security ya kazi kabisa
 
Nasikia yuko StarTV, kule ITV alikuwa anafanya kwa makubaliano maalumu.
Kule ITV Joyce Mhavile alimmwaga. Jamii alipata kijikozi fulani, kurudi akakutana na mhavile ambaye akaammua ammwage. Yupo mitaani
 
Jana usiku nimeona tangazo TBC kipindi kipya cha habari usiku kitarushwa na Jerry Muro na tayari ameshaandaa vipindi kadhaa
 
Jamani,

Jerry Muro ameajiriwa TBC. Alilazimika kuondoka IPP Media (ITV), baada ya jitihada za kumzuia kwenda Marekani kwa kozi fupi kushindikana. Wakubwa zake ITV walijaribu kumzuia, bila ya sababu za msingi na ni kinyume cha jittihada za kuwaendeleza vijana, lakini waliomdhamini, Wamarekani wa USAID, walimpeleka baada ya kuona sababu za kumzuia ni "roho mbaya". Vivyo hivyo kwa kijana mwingine wa ITV, Sudi Mnette, ambaye naye walitaka kumzuia asiende Deutsche Welle, Sauti ya Ujerumani kwa kozi ya miezi sita, lakini akalazimika kuachana na ITV, kwa sababu kama za Jerry Muro na akaenda, akamaliza kozi, sasa ameajiriwa pia na TBC! Hayo ndiyo ya IPP Media na maendeleo ya vijana!

Bwassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…