Jerry Muro, kwa Kiingereza chako hiki, hakika umejidhalilisha na kuwatia aibu mno walimu wako wote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Akiwa anazungumza kwa madaha katika kituo cha Magic fm kipindi katika kipindi chao cha michezo huku muda mwingi akitumia kuiponda Simba, na haswa viongozi wake na haswa akimlenga msemaji mwenzie Haji Manara kuwa hajui kuongea Kiingereza na ndiyo maana Simba haiendi mbali kusajili wachezaji anaowaita yeye " wa kimataifa " na wanaishia tu kusajili wachezaji wa nchi za karibu wanaoongea Kiswahili (hapa akimaanisha wa Uganda, Kenya na Burundi).

Baada ya hapo, Jerry Muro nae, tena mbele ya waandishi wa habari akazungumza Kiingereza hiki nitakachokiandika hapa na alichokuwa anataka kumaanisha kisha tutajua je, ni kweli anajua Kiingereza au ni wale wale? Halafu hapo hapo anasema kuwa ana Master's degree ya Public Administration lakini hatuambii kasoma lini, wapi na kamaliza lini na huku akiwa amesahau kuwa wapo watu wanaomjua a to z au kindakindaki kuliko hata anavyojijua yeye ila tumeamua tu kumfichia siri kwa kumuheshimu kwa kuwa tu ni mwana tasnia mwenzetu.

Kiingereza chake ni hiki kifuatacho na nitaomba sana kama huna background nzuri ya Kiingereza sanifu tusipotezeane muda kwa kubishana bali nataka watakaochangia basi wawe kweli ni wazuri katika communication skills na matumizi ya lugha yenyewe ambayo msemaji wa Yanga, Jerry Muro anasema anaijua huku akidai viongozi wa Simba hawakijui.

Yanga tuko vizuri............yeye akasema............Yanga we are much okey.
Yanga tuko tayari..........yeye akasema............Yanga we are arleady.

Wataalam wa lugha, wajuvi wa Kiingereza cha kuzungumza na kuandika na hata wale mliosoma vizuri sana communication skills, naombeni mnisaidie je, kusema " Yanga we are much okey " na " Yanga we are already " ni Kiingereza sahihi na ambacho mtu wa caliber ya Jerry Muro anaweza kujivunia nacho?

Na namalizia tu kwa kumkumbusha Jerry Muro kuwa, msemaji mwenzie wa Simba Sports Club Haji Manara ni msomi aliyetukuka vizuri tu na haishii tu kuongea Kiingereza kizuri lakini kwa faida yake na wengine msiojua, Haji Manara pia ni linguist tena aliyetukuka.


 
Dah huyu Jerry ni kimbele front awe anatumia tu lugha ya taifa hii lugha ya malikia ni shida tupu.
Yanga we are already. Anatafsiri kiswahili kwenda kingereza ndo mana anachaganya madesa huyu.
 
Unamuonea tu bure

Kama mtu kingereza sio your first langauge
kukosea ni kawaida....
ukianza chunguza kila neno wakati alicho ongea kimeeleweka sio sawa

The BOSS Jaribu Kupata Concept Yangu Kwanza Ndipo Umtetee Mkuu. Nakukubali Mno Ila Katika Hili La Jerry Muro Siko Pamoja Na Wewe. Sasa Kama Wewe Unamtetea Kuwa Kiingereza Kwetu Siyo First Language Iweje Yeye Alikuwa Anamkejeli Haji Manara Kuwa Hajui Kuongea Kiingereza Kama Yeye?

Kwahiyo Hicho Kiingereza Cha Jerry Muro Nilichokiweka Hapo Ndiyo Mahiri? Hata Mdogo Wangu Wa Kike Wa Mwisho Charline Mwenye Miaka 12 Tu Sasa Hawezi Kunitia Aibu Kaka Yake Gentamycine Kwa Kuongea Hicho Kiingereza Kibovu Cha Yanga Mwenzio Jerry Muro Unayemtetea Unless Labda Unataka Kuniaminisha au Kunifanya Nianze Kuhisi Kuwa Pengine Wewe Ndiyo Jerry Muro Mwenyewe.

Pata Concept Yangu Kisha Rejea Content Ya Nini Tunakijadili Hapa Na Hapo Juu Niliweka Angalizo Zuri Tu Kuwa Kama Unajijua Wewe Hauko Vizuri Katika Kukichambua Kiingereza SANIFU Kiwe Cha Kuzungumza au Cha Kuandika Basi TUSICHOSHANE Tafadhali Na Tuwapishe Members Wengine Wanaokijua Wachangie Kimantiki Zaidi.

Nimeweka Uzi Huu Kwa Makusudi Ili Kumpasha Jerry Muro Kuwa Hajui Kiingereza Na Amejichoresha Mbele Ya " Wataalam " Na " Wanataaluma " Wa Lugha Hiyo. Hata Hivyo Akhsante Na Nakushukuru The BOSS Kwa Kuchangia Uzi Wangu " Ki Yanga Yanga ".
 
Kama wewe unajua si ungeweka alichotakiwa kusema?? Ina onyesha na wewe hujui!!!!!
 
Kwaiyo unataka kutuambia wewe unajua kithungu vizuri? Sasa uyo jerry muro ajui english au amekosea kuongea? Mana unatuchanganya ujue brother iyo habari yako yenyewe uliotuletea umeshindwa kufafanua vizuri,jerry muro ajui kiingereza au amekosea kuongea kiingereza? Kwa mfano nikisema jana tulienda na nikasema jana tulikwenda nitakuwa sijui kiswahili au nitakuwa nimekosea kuongea kiswahili vizuri?

Na ninao ongea nao watakuwa wamenielewa au awaja nielewa? Coz inaonekana wazi kuwa alicho ongea jerry muro umemuelewa vizuri nini kamainisha ila sababu una chuki nae ndio umetuletea hoja yako.

Hebu katafute kazi shughuli ya kufanya achana na izo mambo za chuki sisi tumemuelewa vizuri tuu Jerry Muro, hata wewe pia umemuelewa ila roho yako siyo nzuri ndio mana unataka kujifanya unajua Kiingereza
 
Kwanza wewe muongo hiyo hayo mambo kayaongea jana mbele ya vyombo mbali mbali vya habari wakiwemo magic na hakua akiongea na magic peke yao walichofanya magic ni kurakodi tu na kuja kurudia rudia kwenye kipindi chao kwa nia ya kuwakera simba ili nao wajibu hakuna mahali muro kaitaja simba na hiyo ndio tabia hata ya manara akiulizwa kitu kingine lazima ajibu sisi sio kama wale jamaa na watu hutafsiri wale jamaa ni yanga
Huo ndio utamaduni wao kila kitu lazima watanie upande wa pili kwa mafumbo
 
Khaa!! Kama siyo mambo ya uyanga na usimba basi nitasikitika sana kwani wote tunajua Jerry Muro si Muingereza hivyo ni ujinga kusema hajui kiingereza. Anatumia lugha ya mama yake kufikiri kisha kuitafsiri na kuongea kwenye kiingereza.
 
Hata na wewe hujui. Nini maana ya okey? Je, ulitaka kuandika "okay' au? Kama unataka kuongea Kiingereza vizuri ni lazima pia uwe msomaji mzuri wa vitabu vya lugha hiyo. One can be good in spoken but terribly bad in written. Kiswahili chenyewe kinatushinda sembuse Kiingereza?
 
Je hiki

Don't follow follow me without because. Usinifuate fuate bila sababu

Geriii autii get out

Andika hapa ze dogi.Ticha anamfun disha dogo kiingereza yaani the dog

Mzungu anawaaga wabongo byee byee. Mtafsiri wake ana watafsiria Nunua nunua.

You know me and you fotocopy tugeza. Yani tunafanana
 
kama ulikua huna hobby ya kusoma novel tangu uko form two lazima uchapie kwa sana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…