Jerry Silaa: Barabara ya lami ya KM 7.7 yenye thamani ya Tsh Bilioni 9.3 kuunganisha mikoa ya Singida-Simiyu-Arusha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


Wakazi wa Wilaya ya Iramba na Mkalama, Mkoani Singida, wanatarajia kunufaika na barabara ya kiwango cha lami inayojengwa kuunganisha mikoa ya Singida, Simiyu, hadi Arusha. Mradi huu, wenye thamani ya shilingi bilioni tisa, umefikia asilimia 65 ya utekelezaji.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua mradi huo ambao ukikamilika utawasaidia wananchi katika usafirishaji wa mazao ya kilimo, hivyo kuimarisha biashara.

Amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo unaoonesha namna Serikali inavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake bila ubabaishaji.


Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoani Singida, Msama Msama, alieleza kuwa kipande cha barabara kinachojengwa kati ya Kitukutu-Gumanga-Mkalama na Chemchem-Sibiti, kikiwemo Kitukutu-Kinampanda, chenye urefu wa kilomita 7.7, kitagharimu bilioni 9.31 na kinajengwa na mkandarasi mzawa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-23 at 20.30.16_d9ebf322.jpg
    634.8 KB · Views: 4
Hiyo barabara itapunguza mzunguko kwenda bariadi mpaka uende igunga, nzega ukitokea nduguti
 
Mmmmmmmh basi sawa.. hizo pesa nazo zinatolewa hazina wakati halimashauri zingejengewa uwezo zingekuwa zimejenga
 
Shikamoo lami,yaani km 7.7 inagharimu B9? nilijua kichwa habari umekosea kuandika hiyo km7.7 nimejaribu kusoma maelezo yako kumbe ndiyo hiyo hiyo km7.7,hebu tufafanylie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…