Jerry Silaa: Ukiharibu hatukuhamishi bali tutamalizana na wewe

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Jerry Silaa ameonya kwamba mtumishi yeyote wa Umma atakayeharibu hatohamishwa Kituo Bali atamalizana nae Kwa kumfukuza kazi.

Watumishi ujumbe wenu huo

----

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Jerry Silaa @jerrysilaa amesema hakuna Mtumishi yeyote wa ardhi atakayepangiwa eneo jingine la kazi kama atakuwa amekosea katika eneo lake la kazi bali atamaliza nae palepale alipo.

Akiongea akiwa Singida ikiwa ni kuelekea siku 100 tangu kuteuliwa kukamata nafasi hiyo, Waziri Silaa pia ameonya kuhusu Watumishi wazembe wasiotimiza wajibu wao.

“Hakuna yeyote ambaye yupo kwenye Wizara hii ambaye ni mzembe au hatimizi wajibu wake kutokana na vitendo potofu na taaluma yake atahamishwa kutoka eneo moja kwenda jingine, kama kuna Mtumishi hapa singida amefanya jambo baya nitamalizana nae hapahapa”

“Rais ameniamini na kunikasimisha na kumsaidia katika Sekta ya Ardhi ukiharibu Singida tutakuja kumalizana hapahapa Singida, hakuna Mtanzania yoyote asiyekuwa na haki kwamba Mtumishi akiaribu Singida halafu apelekwe kuhamishiwa sehemu nyingine"

Chanzo: Millard
 
Ok! Yetu macho na masikio,muda utaongea!!
 
Back
Top Bottom