Jesca Cox na Nick Vujicic: TAFSIRI ya ubunifu (Creativity), Wanafanya vitu vya kawaida katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Jesca Cox na Nick Vujicic: TAFSIRI ya ubunifu (Creativity), Wanafanya vitu vya kawaida katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Paploman

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,759
Reaction score
3,452
Leo nimepitia vitabu tofauti vikizungumzia maisha na mafanikio ya Nick Vujicic, mlemavu asiyekuwa na mikono Wala miguu na Jesca Cox mwenye ulemavu pia wa mikono( Picha zao nimeambatanisha mwisho wa hili andiko)

Nick Vujicic, Hana mikono Wala miguu lakini ana uwezo wa kuogelea, kuchora na kutembea. Ni motivational speaker, Mpaka Rangi, AirDiver na mhubiri wa neno la mungu.Ana mke na watoto wanne(4).

Nilichojifunza kupitia vitabu hivi;

Hakuna anayeweza kuyabadilisha maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe, Kama wewe mwenyewe hujaamua na kuweka nia ya dhati, Roll model hawatakufanya ufanikiwe.

Inabidi tukubaliane kwamba, kupata mafanikio sio kazi rahisi kunahitaji nguvu na jitahada nyingi sana hadi kufikia kule unakotaka kufika kimafanikio.

Kuna wakati utakatishwa tamaa, kuna wakati utaambiwa huwezi hili au lile, lakini yote hayo yanapotekea yasikukatishe tamaa jipe moyo na endelea kusonga mbele.

Hata Jesca Cox, alikatishwa sana tamaa na wengi na kuambiwa asingeweza kutumiza ndoto yake ya kuwa rubani eti kwa sababu ya ulemavu wake wa mikono.
Leo hii, Jesca ni rubani wa kwanza duniani ambaye hana mikono.


Usikatishe ndoto yako sababu ya maneno ya watu, Kwa sababu unajenga maisha unayoyataka hata kama unapata matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge na kukata tamaa, endelea kuweka juhudi.


Ikiwa unapitia kwenye changamoto nyingi za kimaisha pia acha kukata tamaa, endelea kuweka juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto na kuwa huru.


Ikiwa huridhiki kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye umepoteza, pia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi.


Kwa kila hatua unayochukua kwenye maisha yako hata ikiwa ndogo sana, inaleta mabadiliko kwenye maisha yako. acha kuwasikiliza watu eti kwamba umeshindwa.

Hata upate matokeo mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani lazima juhudi zako zitaleta matunda.
Hakuna mtu katika dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo hayupo.


Hivyo, hata ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa huyaoni.


Kila hatua unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. usikubali hata kidogo kupotezwa na maneno ya watu. Chukua hatua sahihi, ili ufikie mafanikio yako.


Watu wengi mara nyingi huwa wanafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati au ni matokeo ya mapungufu fulani waliyonayo katika maisha, Kama Unaogopa Kufanya Kitu sahihi katika maisha yako, Sahau Kuhusu Mafanikio Katika Maisha Yako Yote.


Fikiria kila unachokijua na kukikumbuka kuhusu mabadiliko unayotaka yawe katika maisha yako, halafu uone ukweli huu


Endelea kupambana na Songa mbele.
FB_IMG_1593967382192.jpg
 
Inspiration!

Tunasubiri na picha zake mkuu.
 
Mimi siamini kabisa ktk hiki kinachoitwa role model, huyo unaemuita role model wako nani alikuwa role model wake? The list goes on, kuwa na role model ni kujiwekea limit ya kifikra na kiutendaji ktk kile unachokipigania, naamini ukichanga karata zako vizuri u can achieve zaidi ya huyo unaemuita role model.
 
Back
Top Bottom