Record Man
JF-Expert Member
- May 25, 2023
- 525
- 876
Siku ya Leo jeshi la Israel lashambuliwa makao makuu ya ujasusi ya Hezbollah ya ujasusi, pia sehemuilikuwa ina sehemu ya kutengenezea mabomu chini ya ardhi.
Jeshi la Israel limesema limefanya shambulizi kwenye makao makuu ya kijasusi ya Hezbollahkatika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
"Mapemaasubuhi ya leo, IAF (kikosi cha anga cha Israel) kilifanya shambulizi kwenyekituo kikuu cha kijasusi cha Hezbollah na eneo la kutengeneza silaha lililokuwachini ya ardhi huko Beirut," jeshi lilisema katika taarifa yake.
Pia limeongeza kuwahatua kadhaa zilichukuliwa ili "kupunguza uwezekano wa kuuawa kwaraia", ikiwemo "kutoa onyo mapema kwa wakaazi".
Jeshi la Israellinasema kikosi chake cha anga kimemuua Al-Haj AbbasSalama, ambaye wanasema ni kamanda mkuu wa Hezbollah katika mstari wa mbele wavita kwenye eneo la kusini, pamoja na Rada Abbas Awada na Ahmad Ali Hussein.
Jeshi hilo pia linasemaAwada alikuwa mtaalamu mkuu wa mawasiliano wa Hezbollah na Hussein aliwahi kuwamkuu wa kitengo cha kutengeneza silaha.Kufikia sasa Hezbollah haijasema chochotekuhusu mashambulizi hayo.
Picha za hivi karibuni kutoka pembezoni mwamji kusini mwa Beirut, zimekuwazikionesha moshi ukiendelea kufuka kwenye majengo ya makaazi ya watu baada yashambulizi la anga la Israel katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
View: https://x.com/bbcswahili/status/1847986196179288287?t=lURaP_KsB6bnyTa5B-WSow&s=19
View: https://youtu.be/qPoJtp2IHbQ?si=i0JKxztjRCg3SrVt